2025
Kama Vile Joseph
Desemba 2024


“Kama vile Joseph,” Rafiki, Januari 2025, 4–5.

Msomaji Rahisi

Kama Vile Joseph

Je, Joseph Smith kweli alimwona Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo?

Hadithi ya kweli kutoka Ufilipino.

Lhensay alijirusha kwenye kiti chake karibu na mama yake wakati basi lao likiendeshwa kupitia mjini. Jumapili ilikuwa siku pendwa ya Lhensay ya wiki! Alipenda kwenda darasa la Watoto na kujifunza kuhusu Yesu Kristo.

Basi lilisimama kwenye stendi yao. Mama alishika mkono wa Lhensay walipokuwa wakitembea kwenda kanisani.

Mama na msichana wakitembea kwenda kanisani

Baada ya mkutano wa sakramenti, Lhensay alitembea kwenda Darasa la Watoto pamoja na Maria rafiki yake. Ubaoni kulikuwa na picha ya kijana akisali msituni.

“Habari ya asubuhi!” Mwalimu wao, Dada Cruz, alionyesha ile picha. “Je, kuna mtu yeyote anamjua huyu ni nani?”

Watoto katika darasa la Msingi

“Huyo ni Joseph Smith!” Lhensay alisema.

Dada Cruz alitabasamu. “Ndio, hiyo ni sahihi. Na Joseph Smith alifanya nini?”

Lhensay alitazama nyuma kwenye picha. Alijua kwamba Joseph Smith alikuwa nabii, lakini hakujua mengine mengi.

“Alikuwa nabii wa kwanza wa kanisa letu,” Maria alisema.

“Sahihi tena!” alisema Dada Cruz. “Wakati Joseph alipokuwa mdogo, hakujua ni kanisa gani la kujiunga nalo. Alikwenda msituni na kuomba kwa Mungu ili kujua ni lipi lilikuwa la kweli. Pia aliomba msamaha wa dhambi zake. Alipokuwa akisali, mwanga mkali sana ulitokea. Je, unajua ni nani aliyekuwa katika mwanga huo?”

Lhensay na wengine wa darasa lake walisubiri.

Dada Cruz aliweka picha nyingine ubaoni. Hii iliwaonyesha wanaume wawili waliosimama juu ya Joseph Smith hewani. Walivaa joho jeupe na kung’ara kwa uangavu.

“Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo walijionyesha kwa Joseph,” Dada Cruz alisema. “Walimwambia kwamba yeye angerejesha Kanisa la Yesu. Na sisi tunaliita Ono la Kwanza.

Lhensay aliinua mkono wake, macho yakiwa wazi. “Je, ilikuwa ni kweli?” aliuliza.

Dada Cruz aliitikia kwa kichwa. “Ndiyo, ilikuwa ni kweli.”

Moyo wa Lhensay ulihisi kuwa na uchangamfu. Alijua kwamba kile Dada Cruz alichikuwa amekisema kilikuwa cha kweli.

Usiku huo, Lhensay aliendelea kufikiria kuhusu Joseph Smith. “Mama, ninawezaje kuwaona Baba wa Mbinguni na Yesu, kama Joseph Smith?” aliuliza.

Msichana akimkumbatia mama yake

Mama alimkumbatia Lhensay. “Wengi wetu hatutamwona Baba wa Mbinguni na Yesu kama Joseph Smith. Lakini bado wanaweza kuzungumza nasi kupitia mawazo na hisia kutoka kwa Roho Mtakatifu. Ndipo utakapojua siku zote Wao wapo pamoja nawe.”

Lhensay alifikiria kuhusu jinsi moyo wake ulivyohisi uchangamfu wakati Dada Cruz alipowaambia kuhusu Ono la Kwanza. Huyo alikuwa Roho Mtakatifu, akituma ujumbe kutoka kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo! Alitabasamu na kumkumbatia Mama. Wao walikuwa wamezungumza naye, kama vile walivyofanya kwa Joseph Smith!

PDF ya hadithi

Vielelezo na Shawna J. C. Tenney