2025
Kumfuata Yesu huko Estonia
Desemba 2024


“Kumfuta Yesu huko Estonia,” Rafiki, Jan. 2025, 10–11.

Kumfuata Yesu huko Estonia

Kutana na Hugo

Mvulana akitazama kandanda

Hugo anamfuata Yesu kwa kusali wakati anapohitaji msaada. Wakati fulani aliota ndoto mbaya. Alisali ili kupokea faraja. “Yesu alinisaidia,” anasema.

Hugo pia anamfuata Yesu kwa kushiriki injili na marafiki zake. Anapenda kuwafundisha kile anachojifunza kanisani. Anawaambia kwamba kila mmoja ni mtoto wa Mungu. “Ninawaalika kanisani na kwenye shughuli,” anasema. “Inanifanya nihisi vizuri.”

Kuhusu Hugo

Mvulana na mama yake wamekaa karibu na kinanda

Umri: miaka 9

Kutoka: Estonia

Lugha: Kiestonia, Kiingereza

Malengo

1) Kuwa bora kwenye kucheza kinanda. 2) Kuwa pamoja milele na familia yake yote, ikijumuisha babu na bibi.

Burudani

  • Kuimba katika Kwaya ya Estonian National Opera Boys

  • Kupiga kinanda

  • Kutumbuiza pamoja na kundi la michezo ya kuigiza

  • Kandanda

Familia: Mama, dada, kaka wawili, na mbwa mwenye jina Ayla

Mambo Ayapendayo Hugo

Mvulana mwenye tabasamu na kielelezo cha kikapu cha Pasaka

Maandiko: 1 Nefi 3:7

Desturi ya Familia: Kuchora na kuficha mayai wakati wa Pasaka

Tunda: Embe

Rangi: Chungwa

Wimbo wa Watoto:A Child’s Prayer” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 12)

PDF ya hadithi

Vielelezo na Suzy Gerhart