Shughuli za :Njoo, Unifuate,” Rafiki, Januari 2025, 22–23.
Shughuli za Njoo, Unifuate
Desemba 30–Januari 5: “Urejesho wa Utimilifu wa Injili ya Yesu Kristo”
Chemsa Biongo ya Urejesho
Kurejesha kitu inamaanisha kukirudisha pamoja tena. Soma “Urejesho wa Utimilifu wa Injili ya Yesu Kristo: Tangazo kwa Ulimwengu la Maadhimisho ya Miaka Mia Mbili” katika Maktaba ya Injili ili kujifunza zaidi kuhusu jinsi Kanisa lilivyorejeshwa. Kisha cheza mchezo wa urejesho! Tafuta au chora picha na uikate katika vipande vya chemsha bongo. Badilishana chemsha bongo na mwanafamilia na rejesheni picha za kila mmoja. Kwa nini ilikuwa muhimu kwamba Joseph Smith arejeshe injili ya Yesu Kristo?
Januari 6–12: Mafundisho na Maagano 1
Mchezo wa Kuganda
Baba wa Mbinguni huzungumza nasi kupitia manabii Wake (ona Mafundisho na Maagano 1:38). Tunahitaji tu kusikiliza! Fanya mazoezi ya kusikiliza kwa kucheza mchezo. Mtu mmoja anapiga muziki, na kila mtu anacheza wakati muziki ukipigwa. Muziki unaposimama, kila mtu huganda. Yeyote atakayeganda mwisho anashiriki sababu moja ya kuwapenda manabii. Endelea mpaka kila mtoto apate zamu ya kushiriki.
Januari 13–19: Joseph Smith—Historia ya 1:1–26
Diorama ya Ono la Kwanza
Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo walimtokea Joseph Smith (ona Joseph Smith—Historia 1:15–20). Tunaliita tukio hili Ono la Kwanza. Nenda kwenye ukurasa wa 13 ili kutengeneza diorama yako mwenyewe ya Ono la Kwanza, na kisha itumie kumsimulia mtu mwingine hadithi hiyo.
Januari 20–26: Mafundisho na Maagano 2; Joseph Smith—Historia ya 1:27–65
Burudani ya Historia ya Familia
Tunapojifunza zaidi kuhusu mababu zetu, tunahisi kuwa karibu nao zaidi na karibu na Baba wa Mbinguni (ona Mafundisho na Maagano 2). Muombe mwanafamilia akusimulie hadithi kutoka kwenye maisha yao au kutoka katika maisha ya mmoja wa mababu zako. Kisha tengeneza tena hadithi hii kama mchezo au mchoro!
Picha na Christina Smith