2025
Mitume Wanatumikia Misioni huko Uingereza
Mei 2025


Hadithi za Maandiko

Mitume Wanatumikia Misioni huko Uingereza

Joseph Smith akivuta taswira akilini ya Mitume wakihubiri huko Uingereza

Bwana alimwambia Joseph Smith kuwatuma baadhi ya Mitume kwenye misioni huko Uingereza. Ilikuwa vigumu kwa Mitume kuacha familia zao, lakini Bwana aliahidi kuwabariki.

Familia ya Kimball wakiwa wagonjwa wamelala kitandani

Heber C. Kimball na mkewe, Vilate, walikuwa na familia changa. Wengi wao walikuwa wagonjwa sana.

Brigham Young akiwaaga familia yake

Brigham Young pia alikuwa mgonjwa, na familia yake ilikuwa masikini. Lakini mke wa Brigham, Mary Ann, alimwambia, “Nenda ukafanye misioni yako, na Bwana atakubariki.”

Heber na Brigham wakiwa nyuma ya mkokoteni

Heber na Brigham walipata nafuu, lakini walikuwa wadhaifu sana. Walitaka kuhubiri injili, hivyo walisema kwaheri kwa familia zao na kupanda nyuma ya mkokoteni kuianza safari yao.

Heber na Brigham wakihubiri injili kwa watu wa Uingereza

Baada ya safari ndefu ya kuvuka bahari, Heber na Brigham waliwasili Uingereza. Pamoja na Mitume wengine, waliwafundisha watu wengi injili. Maelfu ya watu walibatizwa katika Kanisa la Yesu Kristo. Wengi wao walisafiri baharini kujiunga na Watakatifu huko Marekani.

Familia za Heber na Brigham zikiwalaki bandarini

Bwana alitimiza ahadi Yake ya kuzitunza familia za Heber na Brigham wakati walipokuwa wakimtumikia Yeye kama wamisionari.

Ukurasa wa PDF