2025
Kwa Ajili ya Watoto Wakubwa
Mei 2025


Kwa Ajili ya Watoto Wakubwa

Maneno kutoka Kwako

Msichana akitabasamu

Ninahisi furaha ninapomsaidia baba yangu kuwahudumia watu wengine.

Nia L., umri miaka 10, Kaunti ya Hsinchu, Taiwani

Mvulana akitabasamu

Nilisaidia kukata nyasi za uwanja wa jirani yangu. Nilifanya kazi nzuri sana. Ninajua ninapofanya kazi kwa bidii, huwafanya wengine wawe na furaha. Ninajua Baba wa Mbinguni ananipenda.”

Ronin F., umri miaka 10, Utah, Marekani

Ulimwengu wa Mungu wenye rangi nyingi

Baba wa Mbinguni alitupatia ulimwengu mzuri uliojaa rangi. Paka rangi picha kwa kutumia ufunguo hapa chini. Tafuta kila andiko kujua rangi ipi inakwenda kwenye namba husika.

Tapatan

Cheza mchezo kutoka Ufilipino ukiwa na rafiki! Chora ubao wa mchezo kama ule ulio upande wa kushoto. Kila mmoja wenu atahitaji vitu vitatu vidogo, kama mawe au sarafu. Fanyeni zamu kuweka kitu chako kwenye duara. Mara tu vyote vitakapokuwa kwenye ubao, fanyeni zamu kuhamisha kitu chako duara moja katika mwelekeo wowote. Yeyote afunikaye duara tatu mfululizo anashinda!

Msaidizi wa Siri

Mtu kutoka Darasa la Watoto alimshangaza Kaka na Dada Müller kwa kupalilia bustani yao. Lakini huyu alikuwa nani? Fuata vidokezo ili kupata jibu.

  1. Msaidizi wa siri hana mkono ulioinuliwa.

  2. Msaidizi wa siri ana nywele zilizojisokota.

  3. Msaidizi wa siri hajavaa mikanda.

  4. Msaidizi wa siri anatabasamu.

  • Jakob

  • Emelia

  • Lina

  • Felix

  • Tobias

Ukurasa wa PDF wenye shughuli

Vielelezo na Brian Martin