Kutoka Urais wa Kwanza
Mfano wa Mama wa Bibi Yangu
Imetoholewa kutoka “Rahisi Ni Mafundisho ya Yesu Kristo,” Liahona, Nov. 2024, 96–99.
Mama wa bibi yangu Mary Bommeli alijitolea kushiriki injili ya Yesu Kristo. Familia yake ilifundishwa na wamisionari huko Uswizi alipokuwa na umri wa miaka 24.
Baada ya ubatizo wake, Mary alihamia Ujerumani. Aliona kwamba hangeweza kuacha kushiriki mambo ambayo alikuwa amejifunza. Watu walikusanyika kumzunguka ili kumsikiliza akifundisha huku akifuma nguo.
Mary alizungumza juu ya Kitabu cha Mormoni na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kuwa walimtembelea Joseph Smith. Alifundisha kuhusu Ufufuko. Alishuhudia kwamba familia zinaweza kuwa pamoja milele.
Kuwafundisha watoto wa Baba wa Mbinguni kuhusu Yesu Kristo ni kazi takatifu. Tunapofundisha kanuni hizi kwa wale tunaowapenda, Roho Mtakatifu atatusaidia kuujua ukweli huu.
Chora Hadithi ya Familia
Rais Eyring alivutiwa na mama wa bibi yake. Ni nani katika familia yako anakupatia ushawishi wa kuchagua mema? Tumia paneli hapa chini ili kuchora hadithi ya familia.
Kielelezo na Shawna J. C. Tenney