Siyo Kamilifu Sana
Siku kamilifu ya Adeline ilikuwa imekwisha rasmi!
Hadithi ya kweli kutoka Ufaransa.
Adeline alimaliza kuchora kisanduku cha mwisho cha ukaguzi katika karatasi yake. Karibu na hicho, aliandika, Sema sala asubuhi na usiku.
“Hii ni nini?” Maman aliuliza.
“Ninatengeneza orodha ya ukaguzi ya kesho,” Adeline alisema. “Nitakuwa na siku kamilifu!”
Maman aliinua kope za macho yake. “Kweli?”
Adeline ilitikiswa kichwa. “Katika darasa la Watoto tulijifunza kuhusu kukamilishwa katika Kristo. Nitakuwa mwangalifu zaidi ili niweze kuwa na siku kamilifu.”
“Nina furaha unataka kufanya chaguzi nzuri,” Maman alisema. “Lakini unajua, kulikuwa na mtu mmoja tu duniani ambaye alikuwa mkamilifu—Yesu Kristo.”
Adeline aliguna. “Ninajua. Lakini hakika nataka kujaribu! Nafikiri naweza kufanya hivyo.”
Asubuhi ilipofika, Adeline alikuwa tayari. Alitandika kitanda chake na kusema sala yake ya asubuhi.
Wakati wa kifungua kinywa, alisaidia kumlisha dada yake mdogo, Sylvia. Wakati Sylvia alipomwaga pichi zake juu ya kiti chake, Adeline alivuta pumzi ndefu. Alihesabu mpaka nne na alisaidia kusafisha.
Shuleni, Adeline alitafuta watu waliohitaji msaada. Lukas alikuwa ameteguka kifundo cha mguu, hivyo alimbebea trei yake ya chakula cha mchana.
Wakati akiondoka shuleni, Adeline alitoa tabasamu lake kubwa kwa mwanamke aliyefungua lango la shule. Mwanamke huyu kwa kawaida alionekana mwenye chuki. Lakini leo alirudisha tabasamu!
Baada ya shule, Adeline alimpa Sylvia mwanasesere wake pendwa ili achezee. Na kabla ya kwenda kulala, alisema sala. Aliangalia vitu kwenye orodha yake na kuingia kwenye blanketi yake. Alijiona mwenye fahari sana na kuchoka sana. Alikuwa tayari kwa siku nyingine kamilifu kesho!
Wakati Adeline alipoamka siku iliyofuata, wanasesere wake wote walikuwa wamezagaa sakafuni. Sylvia alikuwa amemshika mmoja akimnyonya. Lazima alikuwa amewatoa wote nje!
“Sylvia!” Adeline aliita kwa sauti kubwa. “Nilikuambia usiguse wanasesere wangu!” Alinyakua mwanasesere ambaye Sylvia alikuwa amemshikilia. Sylvia alilia na kukimbia.
Adeline alitazama orodha yake mlangoni. Moyo wake ulididimia.
Maman aliingia ndani wakati Adeline alipohisi chozi kwenye shavu lake.
“Nini kimetokea?” Maman aliuliza.
“Nilisahau kusema sala yangu. Sikutandika kitanda changu.” Sauti ya Adeline ilitetemeka. “Na nilikuwa mkatili kwa Sylvia. Siku yangu kamilifu imekwisha rasmi!”
Maman alimpa Adeline kumbatio. “Ni vigumu sana kuwa mkamilifu wakati wote. Kwa kweli, haiwezekani.”
Adeline alikunja uso. “Lakini basi ninawezaje kuwa mkamilifu katika Kristo?”
“Hiyo ni hivyo tu! Hatuwezi kukamilishwa bila Yesu Kristo,” Maman alisema. “Yeye alitoa uhai Wake kwa ajili yetu kwa sababu Baba wa Mbinguni alijua tungefanya makosa na tungehitaji msaada. Yesu huchukua majaribio yetu yasiyo makamilifu na kuyafanya yawe mazuri zaidi.”
Adeline alifikiria kuhusu hilo. “Kwa hiyo siwezi kuwa na siku kamilifu kila siku?” aliuliza.
Maman alitikisa kichwa chake. “Hapana. Utakuwa na siku ngumu. Lakini utakuwa na siku nzuri pia.” Maman alifunga nywele za Adeline nyuma ya sikio lake. “Wewe jaribu kadiri uwezavyo ndicho kilicho muhimu. Hata kama siku inaanza na uchaguzi mbaya, daima tunaweza kusema sala ya kutubu na kujaribu tena. Kwa msaada wa Yesu Kristo, wewe unatosha.”
Adeline alihisi vizuri moyoni.
“Sasa, kwa ajili ya orodha yako.” Maman alinyosha kidole kwenye ile orodha. “Vipi kuhusu sisi kufokasi tu juu ya jambo moja?”
Adeline aliangalia orodha yake. Alichana sehemu ya ile karatasi na kugundisha kile kilichobaki mlangoni. Kitu kimoja kilichobaki pale kilisema, Sema sala asubuhi na usiku.
Adeline alitabasamu. “Siku yangu yawezekana haikuanza kikamilifu, lakini bado naweza kusema sala sasa. Na kwa msaada wa Yesu Kristo, itakuwa ya kutosha!”
Vielelezo na Giovanni Abeille