Kadi za Mahekalu
Hekalu la Cardston Alberta
-
Hili lilikuwa hekalu la kwanza kujengwa nje ya Marekani.
-
Hekalu hili lina zaidi ya umri wa miaka 100!
-
Hili ni hekalu la kwanza lililosanifiwa bila mnara uliojitokeza juu ya paa.
Hekalu la Taipei Taiwan
-
Hili lilikuwa hekalu la tatu kujengwa huko Asia.
-
Paa la hekalu limefunikwa kwa vigae vizuri vya samawati.
-
Hekalu hili lina minara sita kuzunguka jengo.
Hekalu la Apia Samoa
-
Hili lilikuwa hekalu la kwanza kujengwa huko Samoa.
-
Mwaka 2003, moto uliharibu hekalu hili. Lilijengwa upya mwaka 2005.
-
Sanamu ya malaika Moroni ilikuwa kitu pekee kilichobaki baada ya moto ule. Baadaye iliwekwa kwenye hekalu lililojengwa upya.
Vielelezo na Rachel Erickson