Marafiki kote Ulimwenguni
Rika R., miaka 7, Jimbo la Rewa, Fiji
Brady T., umri miaka 9, Arizona, Marekani
Donghyeon K., umri miaka 10, Seoul, Korea Kusini
Becky na Leo Y., wote wawili wakiwa umri wa miaka 10, Texas, Marekani
Tulivaa, tulicheza michezo ya waanzilishi, tulitengeneza siagi kwenye gudulia, na kutengeneza magari ya kukokotwa na maboksi ili kusherehekea Siku ya Waanzilishi! Tuliwashukuru mababu zetu waanzilishi ambao walivuka nyanda tambarare na walikuwa waaminifu katika injili ya Yesu Kristo.
James, Annie, Alice, na Norah G., umri miaka 7, 9, 3, na 5, Oregon, Marekani
Ninapenda kwenda kanisani kila Jumapili na kuimba nyimbo za Watoto.
Tevin N., umri miaka 7, Harare, Zimbabwe
Kabla hatujaondoka nyumbani kwenda shuleni, ninasema sala yangu ya asubuhi. Ninamshukuru Baba wa Mbinguni kwa ajili yangu, kwa ajili ya mama yangu, na kwa kila kitu.
Carlota V., umri miaka 8, Mkoa wa Lisbon, Ureno
Kujifunza kuhusu waanzilishi kulinipa msukumo wa kutengeneza magari ya kukokotwa na waanzilishi na mikokoteni ya kuvutwa kwa mkono.
Koy S., umri miaka 8, Utah, Marekani
Ninapenda kutengeneza biskuti. Daima ninaongeza kiambato maalumu, ambacho ni upendo! Ninaposhiriki biskuti hizi pamoja na wengine, ninahisi amani na furaha.
Missy N., umri miaka 9, Tennessee, Marekani
Watoto na viongozi katika Mkoa wa Lima, Peru, waliandaa mifuko ya chakula na kuwapa watoto wakimbizi.