2025
Maneno Yangu ya Injili
Mei 2025


Maneno Yangu ya Injili

Tafuta maneno haya na virai katika toleo hili la Rafiki!

Usimamizi

Mikono iliyoishikilia dunia na moyo ukiwa juu yake

Usimamizi ni jukumu la kutunza kitu muhimu. Baba wa Mbinguni anatuamini katika usimamizi wa dunia. Hii inamaanisha kwamba Yeye anatutaka sisi tuutunze na kuulinda ulimwengu Wake mzuri.

Toba

Toba ni jinsi tunavyomgeukia Yesu Kristo pale tunapofanya uchaguzi usio sahihi. Ili kutubu, tunahitaji kusikitika kwa kile tulichofanya, kuomba msaada na msamaha wa Baba wa Mbinguni, na kujaribu kukirekebisha. Kwa sababu ya Upatanisho wa Mwokozi, tunaweza kugeuka kutoka kwenye chaguzi mbaya na badala yake kufanya chaguzi nzuri.

Ufalme wa Selestia

Ufalme wa selestia ni mahali ambapo Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanaishi. Kwa kuchagua kumfuata Yesu Kristo, tunaweza kuishi huko siku moja pamoja na familia zetu milele.

Ufufuko

Mvulana amesimama kando ya mstari wa kuonyesha umbo la mwili wake

Ufufuko ni wakati roho na mwili wako vinaporudi pamoja baada ya kufa kwako. Mara unapofufuka, mwili wako ni mkamilifu, na huwezi tena kuugua au kufa. Kwa sababu ya Upatanisho wa Yesu Kristo, kila mtu atafufuka.

Ukurasa wa PDF

Vielelezo na Madison Baker