2025
Kumfuata Yesu huko Taiwani
Mei 2025


Kumfuata Yesu huko Taiwani

Kutana na Ellie

Msichana akitabasamu

Ellie anamfuata Yesu Kristo kwa kuisaidia familia yake kufanya shughuli za jioni ya nyumbani. Alimfundisha mdogo wake wa kiume na dada yake makala ya nne ya imani kwa shughuli moja. Alikariri makala ya imani kwa kuirudia rudia wakati wa mchana. “Kufanya hili kunaweza kunisaidia kuja hatua moja karibu na Kristo,” Ellie anasema.

Ellie ni mpatanishi katika familia yake. Anamsaidia mdogo wake wa kike kuvaa viatu vyake na kumlisha wakati mama yake anapokuwa na shughuli nyingi. Wakati ndugu zake wadogo wanapogombania zawadi au kiti, anashiriki nao. Ellie anasema, “Mimi ninapomfuata Yesu, ninajisikia vizuri moyoni mwangu.”

Kuhusu Ellie

Msichana akiendesha skuta wakati mama yake na mdogo wake wa kike wakitembea nyuma yake

Umri miaka: 7

Kutoka: Taoyuan, Taiwani

Lugha: Kitaiwani, Kimandarini, Kiingereza

Malengo: Kupiga kinanda vizuri sana, kujifunza Makala za Imani, kujifunza mpira wa vinyoya

Mambo Ayapendayo: Kupiga kinanda, sanaa na ufundi, kupanda mwamba, kuimba

Familia: Ellie, Mama, Baba, kaka mdogo, dada mdogo

familia ikitabasamu

Mapendeleo ya Ellie

Baba na binti wakiangalia maandishi ubaoni

Hadithi ya Maandiko: Nefi akijifanya kuwa Labani ili kupata mabamba ya shaba (ona 1 Nefi 4)

Matunda na mboga: Mapichi matamu, zabibu, na uyoga wa enoki

Chakula: Tambi za kupika muda mfupi

Rangi: Upinde wa mvua

Wimbo wa Watoto:Families Can Be Together Forever” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 188)

Familia ikitazama kitabu pamoja
Ukurasa wa PDF