2025
Salamu kutoka Taiwani
Mei 2025


Salamu kutoka Taiwani!

Taiwani ni kisiwa karibu na Hong Kong. Zaidi ya watu milioni 23 wanaishi huko. Lugha zinazozungumzwa zaidi ni Kimandarini, Kihokieni, na Kihaka.

Muda wa Kulala!

Nchini Taiwani ni kawaida mashuleni na ofisini kuwa na muda mfupi wa kulala baada ya chakula cha mchana.

Ua Maalumu

Maua ya plamu yamekuwa ishara rasmi ya Taiwani tangu mwaka 1964. Walilichagua kwa sababu linachanua hata wakati wa majira ya baridi.

Kasi ya Lifti

Taipei 101 ni jengo refu zaidi nchini Taiwani. Lina lifti ya haraka sana ambayo inachukua sekunde 37 tu kutoka ghorofa ya 5 hadi ya 89.

Milima Mingi

Zaidi ya nusu ya Taiwani imefunikwa katika milima. Pia kuna volkano kadhaa, lakini hazijalipuka kwa mamia ya miaka.

Upinde wa Mvua wa Kupendeza

Upinde wa mvua uliodumu kwa muda mrefu zaidi duniani ulitokea nchini Taiwani. Watu wangeweza kuuona kwa takribani saa tisa!

Sherehe ya Kandili ya Angani

Tamasha la Kandili la Taiwani ni ishara ya matumaini, shangwe, na umoja. Wakati wa tamasha hili kubwa, watu hutengeneza kandili na kuzirusha angani.

Ukurasa wa PDF

Vielelezo na Kitabu cha Lai