Tuendelee Kusonga Mbele
Mchezo wa Kurusha Haraka
-
Chagua kitu laini cha kurusha, kama jozi ya soksi zilizofungwa, mpira laini, fulana—kitu chochote!
-
Ketini katika mduara na wekeni kipima muda kwa sekunde 30. Rusha kitu hicho kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mtu mwingine haraka kadiri muwezavyo. Wakati kipima muda kinapolia, yeyote ambaye ana kitu kile anatoka mchezoni.
-
Anzisha kipima muda na chezeni tena na tena mpaka mtu mmoja atakapobakia. Mtu wa mwisho anashinda! Unaweza pia kucheza mchezo huu kwa muziki kwa kuupiga na kuusimamisha bila mpangilio. Yeyote anayekuwa na kitu wakati muziki unaposimama anatoka mchezoni, na mtu wa mwisho ndiye mshindi.
Kielelezo na Yev Haidamaka