Shughuli za Njoo, Unifuate
Juni 30–Julai 6: Mafundisho na Maagano 71–75
Mioyo ya Huduma
Mungu anawaita maaskofu na marais wa matawi ili kusaidia kuwahudumia watu katika kata au matawi yao (ona Mafundisho na Maagano 72:2). Kata mioyo ya karatasi na uandike vitu unavyopenda kuhusu askofu wako au rais wa tawi juu ya kila mmoja. Gundisha mioyo hiyo kwenye mlango wa ofisi au nyumba yao.
Julai 7–13: Mafundisho na Maagano 76
Jua la Selestia
Siku moja tunaweza kuishi katika ufalme wa selestia pamoja na Baba wa Mbinguni, Yesu Kristo, na familia zetu (ona Mafundisho na Maagano 76:62, 70, 92). Maandiko yanafananisha ufalme wa selestia na jua. Tumia sahani ya karatasi au kipande cha karatasi kutengeneza jua. Kata pembetatu za karatasi kwa ajili ya miale ya jua na zigundishe au zibandike kwenye duara. Zungumza kuhusu kile unachoweza kufanya sasa ili kujiandaa kuishi na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo siku moja.
Julai 14–20: Mafundisho na Maagano 77–80
Matendo ya Wanyama
Chini ya maelekezo ya Mungu, Yesu Kristo aliumba kila kiumbe duniani (ona Mafundisho na Maagano 77:2). Chezeni mchezo wa kubashiri mnyama! Mtu mmoja anajifanya kuwa mnyama fulani. Kila mtu mwingine anajaribu kubashiri ni wanyama gani hao. Mara unapobashiri kwa usahihi, sema kitu unachokipenda kuhusu mnyama huyo.
Julai 21–27: Mafundisho na Maagano 81–83
Imba na Sali
Baba wa Mbinguni daima husikia sala zetu (ona Mafundisho na Maagano 81:3). Pamoja na familia yako, imbeni “A Child’s Prayer” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 12). Anza wimbo na mtu mmoja tu. Kisha pole pole kila mtu ajiunge. Baada ya kuimba, zungumzeni kuhusu mambo mnayoweza kuyaombea kama familia.
Picha na Christina Smith