Ulimwengu Wetu wa Kupendeza
Imetoholewa kutoka “Usimamizi Wetu wa Ulimwengu,” Liahona,, Nov 2022, 57-59.
Mimi na mke wangu tuliwachukua wajukuu zetu wachache kwenda kwenye bustani nzuri sana huko Ufaransa. Tulipendezwa na matuta mazuri ya maua, maua ya maji, na mabwawa.
Bustani ilikuwa mali ya mtu aitwaye Claude Monet. Alikuwa mchoraji maarufu. Kwa makini alifanya kazi kwenye bustani yake kwa miaka 40. Alitengeneza mamia ya michoro ambayo ilitokana na uvuvio wa bustani yake.
Uzuri wa asili unaweza kutusaidia kuwa na shukrani kwa Baba yetu wa Mbinguni na Mwanawe, Yesu Kristo. Waliumba dunia hii nzuri na milima, mito, mimea, na wanyama.
Uumbaji huu wa kustaajabisha unaonyesha ni kiasi gani Mungu anatupenda. Hata hivyo, uumbaji pia huja na kazi na majukumu. Hii inaitwa usimamizi. Tunahitaji kutunza vitu ambavyo Mungu ameumba kwa ajili yetu.
Baba yetu wa Mbinguni pia anatualika tujiunge katika kazi Yake ya ubunifu. Tunaweza kutengeneza sanaa, muziki, na vitu vingine ili kuangaza maisha yetu na kuwabariki wengine.
Mungu anaahidi baraka kuu wakati tunapoipenda na kuitunza dunia na kutunzana sisi kwa sisi. Unapofanya hivyo, utahisi upendo Wake zaidi katika maisha yako.
Sanaa ya Karatasi Iliyochanika
Askofu Caussé alifundisha kwamba sisi pia tunaweza kuwa waumbaji! Hapa kuna sanaa ya ufundi unayoweza kutengeneza ili kukukumbusha juu ya uumbaji mzuri wa Baba wa Mbinguni.
-
Tafuta picha ya kitu fulani katika mazingira ya asili ambacho kinakuvutia wewe.
-
Kwenye kipande cha karatasi, tumia penseli kuchora sehemu tofauti tofauti za hiyo picha.
-
Chana karatasi iliyopakwa rangi ili kuitumia katika picha yako.
-
Gundisha vipande vya karatasi vilivyopakwa rangi ndani ya mchoro wako.
Vielelezo na Maddie Baker