2025
Tukio la Safari ya Msituni
Mei 2025


“Tukio la Safari ya Msituni,” Rafiki, Mei 2025, 40–41.

Tukio la Safari ya Msituni

“Hebu tuchomoke kwenye kundi,” Ralph alisema.

Hadithi ya kweli kutoka Ghana.

Kundi la watoto wakiwa wamesimama mbele ya ishara ya jiwe

Nyamedo alikimbilia basi akiwa na kaka yake mdogo, Kwame. Walipanda ngazi na kuketi karibu na dirisha. Nyamedo alitazama nje kuona jua likiangaza kwenye miti ya kijani. Shule yao ilikuwa ikienda kwenye safari ya msituni kwenye hifadhi ya asili. Leo ingekuwa tukio la ugunduzi!

“Halo, Nyamedo!”

Marafiki wa Nyamedo, Ralph na Sierra walikaa kwenye kiti upande mwingine kutoka kwake.

Ralph alivuta kwenye mkono wa shati ya Nyamedo na kunong’ona. “Tunakifika kwenye hifadhi, twende kwenye uvumbuzi!”

“Ndiyo!” Sierra alisema. “Tunaweza kuwa na tukio letu wenyewe la ugunduzi.”

Ralph alikubali kwa kichwa kwa msisimko. “Tunaweza kuchomoka kabla ya shughuli ya kwanza.”

Nyamedo alifikiria mambo yote ambayo wangeweza kuyaona nyikani. Miti mirefu, wanyama wazuri, na pengine maporomoko ya maji!

“Hiyo inaonekana kuwa ya kufurahisha! Acha tufanye hivyo,” alisema kwa tabasamu.

Wakati basi lilipofika kwenye hifadhi ya asili, Nyamedo na Kwame walishuka kutoka kwenye basi pamoja. Walimu wao walimwambia kila mtu abaki na kundi na asizurure.

Ralph alitembea hadi kwa Nyamedo. “Unaukumbuka mpango?” Ralph alinong’ona.

Nyamedo alikubali kwa kichwa. Lakini kisha akaacha kufikiria. Kutafiti nyika kulionekana kusisimua, lakini Nyamedo pia alijua inaweza kuwa hatari. Vipi kama wangepotea au kuumia?

Ghafla, alihisi sauti ikizungumza naye. Baki na Kwame.

Sauti ilikuwa tulivu na ndogo. Nyamedo alijua alikuwa ni Roho Mtakatifu.

Alikuwa na wasiwasi kwamba marafiki zake wangemkasirikia kwa kutotafiti pamoja nao. Lakini pengine Roho Mtakatifu alikuwa akimlinda.

Nyamedo alimgeukia Ralph. “Samahani, kwa kweli ninapaswa kubaki na kaka yangu,” alisema. “Yeye ni jukumu langu.”

Ralph alinuna.

“Lakini ulisema ungekuja!”

“Mwalimu alisema tunapaswa kubaki,” Nyamedo alisema. Ralph alivuta pumzi na kuondoka.

Mvulana akiteleza kwa kamba na kutazama ndege

Nyamedo na Kwame walikwenda na wanafunzi wengine na kuwafuata walimu wao. Kwanza walienda kwenye kamba ya kuteleza. Upepo ulivuma dhidi ya nyuso zao walipokuwa wakipita juu ya miti ya kijani. Ilikuwa kama kuruka angani!

Mvulana akipanda miamba na akiendesha farasi

Kisha viongozi katika hifadhi waliwafundisha kuhusu baadhi ya wanyama ambao waliishi huko. Nyamedo na Kwame hawakuweza kusubiri kuwaona. Walijifunza kuhusu punda milia, nyani, nyoka, swala, na ndege wengi! Baada ya kuona wanyama wote wazuri, walikwenda kupanda miamba na kuendesha farasi. Baadaye walicheza michezo.

Nyamedo alikuwa na furaha kwamba alikuwa amebaki na Kwame. Kama asingefanya hivyo, angekosa vitu vingi vya kufurahisha!

Ilipofika muda wa kurudi kwenye basi, Nyamedo aliwaona Ralph na Sierra. Walimkimbilia.

“Karibu tufukuzwe na nyani wenye hasira,” Ralph alinong’ona. Alionekana kuwa na hofu kidogo. “Tungeweza kuumizwa.”

Sierra aliitikia kwa kichwa. “Ni vizuri wewe hukuja.”

“Wee,” alisema Nyamedo. “Ninafurahi kuwa mko SAWA!”

Roho Mtakatifu kweli alikuwa ananilinda, aliwaza. Aliushika mkono wa Kwame walipokuwa wanaingia kwenye basi pamoja.

Alikuwa na shukrani kwamba Roho Mtakatifu alikuwa amewaweka salama na kuwasaidia kuwa na tukio la kufurahisha.

PDF ya hadithi

Vielelezo na Cam Kendell