2025
Margo na Paolo
Mei 2025


“Margo na Paolo,” Rafiki, Mei 2025, 33.

Margo na Paolo

Sauti Ndogo, Tulivu

Margo akiwa na Kiwi juu ya kichwa chake, akiwa amekaa kwenye benchi nje ya nyumba, wakati Bibi akija kwenye kibaraza duara akiwa na kopo la kumwagilia

Ee, ninawaona ninyi wawili mpo kwenye eneo lenu la kufikiri. “Mnafikiria kuhusu nini leo?”

Roho Mtakatifu.

Bibi na Margo wakizungumza

Watu wanasema Yeye anazungumza nao kwa sauti tulivu. Lakini mimi sijawahi kumsikia Yeye! Je, wewe?

Bibi akimwagilia maji mmea wakati akizungumza na Margo

Siyo kwa masikio yangu. Lakini ninamsikia Yeye kwa moyo wangu.

Unamaanisha nini?

Picha ya karibu sana ya Bibi

Vema, Roho Mtakatifu kwa kawaida huzungumza nasi kupitia mawazo na hisia zetu.

Bibi akimwagilia mmea wakati Margo akizunguka kwenye benchi ili kuzungumza naye

Nilipohisi kama sipaswi kwenda jiu jitsu siku ya Jumapili, huyo alikuwa ni Roho Mtakatifu?

Nadhani hivyo! Roho Mtakatifu hutusaidia kufanya chaguzi nzuri na kuhisi amani.

Margo akifikiria na kisha kuegemea nyuma kwa amani macho yake yakiwa yamefumbwa

Nadhani Yeye anazungumza nami! Lazima nisikilize tu.

Ukurasa wa PDF wa hadithi aina ya vichekesho

Vielelezo na Katie McDee