“Kujifunza kutoka kwenye Mkutano mkuu” Rafiki, Mei 2025, 1.
Kujifunza kutoka kwenye Mkutano Mkuu
Kutumainia Hekaluni
Fuata mzingile ili kufika hekaluni. Je, unatarajia nini kuhusu kwenda hekaluni siku moja?
Kusikiliza Mkutano Mkuu
Kwenye mkutano mkuu familia yangu na mimi tunaweka alama kwenye bakuli zenye pipi kwa maneno kama imani, hekalu, na sala. Tunaposikia moja ya maneno haya, tunaweza kuchukua pipi kutoka kwenye bakuli lake. Maneno haya yananisaidia kumfikiria Yesu na kusikiliza hotuba.
Jane C., umri miaka 6, Quebec, Kanada
Ninapenda mkutano mkuu kwa sababu kupitia hotuba ninaweza kumhisi Roho Mtakatifu na kujifunza zaidi kuhusu Yesu Kristo.
Tomas P., umri miaka 8, Buenos Aires, Argentina
Njooni kwa Kristo
Mzee Gary E. Stevenson alifundisha kwamba ishara ya Kanisa inatukumbusha kwamba Kristo ndiye kiini cha Kanisa letu na anapaswa kuwa kitovu cha maisha yetu pia.
Chora mstari ili kuoanisha maelezo na kila sehemu ya ishara.
-
Jiwe la pembeni ni jiwe muhimu zaidi katika msingi wa jengo. Jina la Kanisa lipo ndani ya jiwe la pembeni kutukumbusha kwamba Yesu Kristo ndiye jiwe Kuu la Pembeni.
-
Mikono iliyonyoshwa ya Mwokozi inawakilisha ahadi Yake ya kuwakumbatia wote wanaokuja Kwake.
-
Tao ambapo Yesu Kristo anasimama chini yake inawakilisha wakati alipotoka kaburini, akiwa amefufuka. Yu hai, na sisi tunamfuata Yeye!
Vielelezo na Josh Talbot