“Maneno Yangu ya Injili,” Rafiki, Mei 2025, 10.
Maneno Yangu ya Injili
Tafuta maneno haya na virai katika toleo hili la Rafiki!
Amri
Amri ni kitu ambacho Baba wa Mbinguni anatutaka tufanye kwa sababu Yeye anatupenda. Amri ni maelekezo ambayo Yeye hutupa sisi ili tuweze kuwa na furaha na kurudi Kwake siku moja. Tunabarikiwa tunapofuata amri Zake.
Vipawa vya Kiroho
Kupitia Roho Mtakatifu, Baba wa Mbinguni humpa kila mmoja wetu kipawa cha kiroho ili kuwabariki wengine. Si kila mtu ana vipawa sawa, lakini kila mtu ana kipawa cha kiroho kutoka kwa Mungu. Unaweza kusoma kuhusu baadhi ya vipawa hivi katika Mafundisho na Maagano 46:11–26.
Ushuhuda
Ushuhuda ni kile unachoamini au kujua kuwa ni kweli kuhusu Baba wa Mbinguni, Yesu Kristo, na injili Yao.
Uzima wa Milele
Shukrani kwa Upatanisho na Ufufuko wa Yesu Kristo, tunaweza kupata uzima wa milele, ambayo inamaanisha tutaishi milele na Baba wa Mbinguni, Yesu, na familia zetu.
Vielelezo na Madison Baker