“Ushuhuda juu ya Yesu,” Rafiki, Mei 2025, 11. Majibu kutoka kwa Mtume Ushuhuda Juu ya Yesu Na Mzee D. Todd Christofferson Wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili Imetoholewa kutoka “Ushuhuda juu ya Yesu,” Liahona, Mei 2024, 97–100. Ushuhuda juu ya Yesu ni kujua kwamba Yeye ni Mwana mtakatifu wa Mungu, Masiya na Mkombozi. Ushuhuda wetu unaonyeshwa na yule tunayekuwa. Tunaweza kuimarisha ushuhuda wetu kwa kusali, kujifunza maandiko na kuitakasa siku ya Sabato. Fungua PDF Vielelezo na Mark Robison