“Mary na Caroline Wanaokoa Maandiko,” Rafiki, Mei 2025, 26–28.
Hadithi za Maandiko
Mary na Caroline Wanaokoa Maandiko
Mary Rollins alikuwa na umri wa miaka 12 wakati alipojifunza kwa mara ya kwanza kuhusu Kitabu cha Mormoni. Aliazima nakala na kuendelea kusoma usiku mzima.
Mary pia alifurahia kitabu kipya kilichoitwa Kitabu cha Amri. Kingekuwa na mafundisho mengi ambayo Yesu Kristo alikuwa ameyatoa kwa Joseph Smith.
Lakini baadhi ya watu hawakulipenda Kanisa. Siku moja, wanaume walivunja jengo ambapo Kitabu cha Amri kilikuwa kikichapishwa. Walitupa mashine ya uchapishaji nje ya dirisha na kutawanya kurasa mtaani.
Mary na dada yake mdogo, Caroline, walijificha na kuangalia. Mary alitaka kuokoa kurasa kabla hazijaharibiwa. Caroline alikuwa na hofu, lakini walijua kurasa zilikuwa na neno la Mungu juu yake.
Akina dada walikimbia mtaani na kunyakua kurasa nyingi kadiri wawezavyo. Baadhi ya watu waliwaona na kuwapiga kelele ili waache. Mary na Caroline walishikilia kurasa kwa nguvu zaidi na kukimbia kwenye shamba la mahindi lililokuwa karibu.
Watu wawili waliwafukuza. Mary na Caroline walianguka ardhini na kuficha kurasa chini ya miili yao. Walisikiliza kwa utulivu wakati wanaume wakiwatafuta.
Punde wanaume wakaacha kutafuta. Mary na Caroline walikuwa salama! Walikuwa wameokoa kurasa. Leo mafundisho hayo yako katika Mafundisho na Maagano.