2025
Nifundishe Kuhusu Roho Mtakatifu
Mei 2025


“Nifundishe Kuhusu Roho Mtakatifu,” Rafiki, Mei 2025, 46–47.

Misingi ya Injili

Nifundishe Kuhusu Roho Mtakatifu

Roho Mtakatifu ni roho. Hiyo inamaanisha Yeye hana mwili wa kushikika. Yeye hutusaidia kujua kile Baba wa Mbinguni anachotaka kutuambia.

Roho Mtakatifu anaweza kutufariji wakati tunapokuwa na hofu au huzuni. Anaongea nasi kwa hisia tulivu na mawazo.

Roho Mtakatifu hutusaidia tuhisi furaha wakati tunapofanya chaguzi nzuri.

Roho Mtakatifu hutusaidia kuhisi upendo kutoka kwa Baba yetu wa Mbinguni na Yesu Kristo. Yeye hutusaidia tujue kile kilicho kweli.

Wakati wa Shughuli

Roho Mtakatifu anaweza kukusaidia na kukuongoza kufanya chaguzi nzuri. Onesha kwa kidole chaguzi nzuri watoto hawa wanazofanya.

Ukurasa PDF ukiwa na shughuli

Vielelezo na Tracy Walker