2025
Kutembea katika Nyayo Zake
Mei 2025


“Kutembea katika Nyayo Zake,” Rafiki, Mei 2025, 17.

Imeandikwa na Wewe

Kutembea katika Nyayo Zake

Kielelezo cha mzee akitembea kwenye theluji wakati mvulana na msichana wakitembea katika nyayo zake nyuma yake

Siku moja familia yangu ilienda kuteleza na sleji pamoja na bibi na baba yangu. Tulitembea hadi kwenye eneo lililokuwa limefunikwa kwa futi kadhaa za theluji safi. Ilikuwa vigumu sana kutembea ndani! Dada yangu alikuwa na wakati mgumu kutembea katika theluji, hivyo baba yangu alisema, “Tembea tu katika nyayo zangu.”

Mimi na dada yangu tulianza kukanyaga nyayo zake. Baada ya muda nilitaka kujaribu kutembea peke yangu kwa muda kidogo. Nilipotembea peke yangu kwenye theluji, ilikuwa ni vigumu zaidi!

Kutembea katika nyayo za baba yangu ilikuwa rahisi kwa sababu tayari alifanya sehemu ngumu ya kutembea kwenye theluji. Nina ushuhuda kwamba Yesu Kristo tayari alifanya sehemu ngumu zaidi. Kama utatembea katika nyayo za Yesu, maisha yako yatakuwa rahisi pia.

alt text

Kielelezo na Abby Rummler