“Karibuni, Marafiki!” Rafiki, Mei 2025, 1.
Karibuni, Marafiki!
Nabii anatufundisha jinsi ya kumfuata Yesu Kristo. Fungua ukurasa ili kusoma kile alichofundisha kwenye mkutano mkuu.
Roho Mtakatifu pia hutuongoza sisi. Kwenye ukurasa wa 8, soma jinsi Marcie alivyomhisi Roho Mtakatifu wakati akiendesha baiskeli yake. Roho Mtakatifu alimsaidia Nyamedo kufanya uchaguzi mzuri kwenye safari ya shule (ukurasa wa 40). Kama utamsikiliza Roho Mtakatifu, unaweza kuhisi jumbe ambazo zinakufariji, kukuongoza, na kukufundisha.
Daima kumbuka kwamba una msaada kutoka kwa manabii, Roho Mtakatifu, na wengine wanaokupenda!
Kwa upendo,
Rafiki
Tafadhali: Tuambie kuhusu wakati ulipomsikiliza nabii au kumfuata Roho Mtakatifu.