“Kadi za Mahekalu,” Rafiki, Mei 2025, 16.
Kadi za Mahekalu
Hekalu la Tokyo Japan
-
Liliwekwa wakfu mnamo 1980 na lilikuwa hekalu la kwanza huko Asia!
-
Ndani kuna mifumo ya jadi ya Kijapani katika vitambaa na vioo.
-
Mnamo 1949 Mtume alitoa unabii kwamba mahekalu yatajengwa huko Japani. Sasa Japan ina manne!
Hekalu la Phnom Penh Cambodia
-
Hili litakuwa hekalu la kwanza huko Cambodia!
-
Kuna zaidi ya waumini 16,000 wa Kanisa huko Cambodia.
-
Wakati wa ziara ya kwanza ya Rais Nelson kule Cambodia, alishiriki picha ya jinsi ambavyo hekalu hili lingeonekana.
Hekalu la Copenhagen Denmark
-
Kwanza lilijengwa kama kanisa dogo, kisha likageuka kuwa hekalu miaka 73 baadaye.
-
Hekalu lina mlango wa mwanzoni wa kanisa na matofali mekundu.
-
Kuna mnara karibu na hekalu pamoja na malaika Moroni juu.
Vielelezo na Rachel Erickson