“Kujiamini mbele za Mungu,” Rafiki, Mei 2025, 02–03.
Ujumbe wa Mkutano kutoka kwa Nabii
Kujiamini mbele za Mungu
Imetoholewa kutoka kwenye “Kujiamini katika Uwepo wa Mungu,” Liahona, Mei 2025, 127–29.
Tunapofanya na kushika maagano, tunaweza kuwa na kujiamini kutoka kwa Roho Mtakatifu. Tunaweza kuwa na kujiamini kwamba Baba wa Mbinguni anatusikia na anatupenda zaidi ya tunavyoweza kuelewa. Tunaweza kuwa na kujiamini kwamba Yeye anataka kutusaidia kufikia uwezekano wetu wa juu zaidi. Hisani na wema hufungua njia ya kujiamini mbele za Mungu!
Hisani kwa wote ni alama ya wapatanishi! Acha tuombe kwa Baba wa Mbinguni ili tujaze mioyo yetu na hisani.
Wema hufanya kila kitu kuwa bora na chenye furaha zaidi! Kama una wazo baya, wazo la kikaltili, au wazo la huzuni, wema utaondoa mawazo hayo.
Mawazo yetu, maneno, na matendo yetu yanahitaji kujazwa na wema na upendo msafi wa Kristo kwa watu wote. Ninawaalika mkue katika kujiamini kwenu mbele za Bwana.
Jifunze
Chora au andika majibu yako kwa maswali haya kuhusu ujumbe wa Rais Nelson.
-
Je, unawezaje kuonesha upendo na hisani kwa wengine?
-
Ni kitu gani kilicho kizuri unachoweza kufikiria kama wazo baya, katili, au la kuhuzunisha linakuja akilini mwako?
Ni andiko lipi Rais Nelson alitumia kufundisha kuhusu hisani na wema? (Dokezo: Unaweza kutumia maandiko yako ili kuangalia juu!)
-
Waebrania 11:1
-
Amosi 3:7
Kielelezo na Josh Talbot