“Shughuli za Njoo, Unifuate,” Rafiki, Mei 2025, 22–23.
Shughuli za Njoo, Unifuate
Kwa ajili ya jioni ya nyumbani, au kujifunza maandiko—au kwa ajili ya burudani tu!
Aprili 28–Mei 4: Mafundisho na Maagano 41–44
Taa Nyekundu, Taa ya Kijani
Maandiko yanafundisha jinsi ilivyo muhimu kufuata amri za Mungu ( ona Mafundisho na Maagano 42). Acha mtu mmoja awe kiongozi na asimame mbele ya kundi. Wanaposema “taa ya kijani,” kila mtu anaweza kusonga mbele. Wanaposema “taa nyekundu,” kila mtu anatakiwa kuganda!
Mei 5–11: Mafundisho na Maagano 45
Tarumbeta ya Malaika
Malaika atapiga tarumbeta wakati Yesu Kristo atakapokuja tena ( ona Mafundisho na Maagano 45:45). Tengeneza tarumbeta yako mwenyewe ya karatasi! Bingirisha kipande cha karatasi katika umbo la pia na uifunge kwa gundi. Unaweza pia kuongeza mshikio kwenye tarumbeta yako au duara kwa ajili ya vifungo. Kisha fanya mazoezi ya kuzungumza katika tarumbeta yako na kusema kwa nini unampenda Yesu Kristo.
Mei 12–18: Mafundisho na Maagano 46–48
Kombe la Ukarimu
Mungu humpa kila mtu vipawa vya kiroho. Hiyo inamaanisha Yeye hutubariki kwa talanta kupitia Roho Mtakatifu (ona Mafundisho na Maagano 46:11–33). Tafuta chupa tupu au kikombe. Kwenye vipande vya karatasi, andika talanta au vipawa tofauti ambavyo mtu anaweza kuwa navyo. Fanya zamu kuchagua kutoka kwenye chupa na kumtaja mtu unayemjua ambaye ana kipawa hicho!
Mei 19–25: Mafundisho na Maagano 49–50
Fuata Njia
Injili ya Yesu Kristo mara nyingi huitwa agano lisilo na mwisho (ona Mafundisho na Maagano 49:9, 12–14). Rais Nelson pia ameiita njia ya agano. Kwenye vipande kadhaa vya karatasi, andika njia tunazoweza kumfuata Yesu Kristo. Tengeneza njia kwa karatasi na fanyeni zamu kutembea juu yake.
Picha na Christina Smith