“Vidokezo kwa ajili ya Safari Yako ya Kwanza ya Hekaluni,” Rafiki, Novemba 2024, 38–39.
Vidokezo kwa ajili ya Safari Yako ya Kwanza ya Hekaluni
Ndani ya hekalu, unaweza kubatizwa na kuthibitishwa kwa niaba ya watu waliokufa bila kupata injili. Watu hao watakuwa na nafasi ya kufanya agano na Mungu na kupokea baraka Zake, kama vile wewe ulivyofanya wakati ulipobatizwa na kuthibitishwa.
Kitu cha Kubeba
-
Mavazi ya Kanisani (zivae kwenda hekaluni)
-
Kibali cha hekaluni
-
Brashi ya Nywele na tai ya nywele (kama itahitajika)
-
Majina ya familia yaliyochapishwa kutoka kwenye app ya FamilySearch au tovuti (kwa hiari)
Nini cha Kufanya
1. Ingia Hekaluni
Onyesha kibali chako kwenye dawati la mbele. Kisha unaweza kwenda mahali pa kubatiza. Mfanyakazi wa hekalu atakupa nguo za ndani nyeupe, soksi na jampsuti ya ubatizo.
2. Badilisha Mavazi Yako
Katika chumba cha kuvalia, badilisha nguo na uvae ulizopewa. Weka vitu vyako kwenye kabati tupu. Kisha funga kabati yako kwa ufunguo na tunza ufunguo kwenye jampsuti yako. Kama una nywele ndefu, funga kwa nyuma. Weka majina ya familia yako yaliyochapishwa pamoja nawe.
3. Subiri kwa staha
Unaposubiri zamu yako ya kubatizwa, unaweza kusoma maandiko, kusali au kutafakari. Unaweza pia kufikiria kuhusu watu utakaobatizwa kwa niaba yao.
4. Shiriki katika Ubatizo wa Hekaluni
Inapofika zamu yako, toa majina ya familia yako kwa mtu aliye kwenye dawati. Kama hauna majina, watatumia majina ya hekaluni badala yake. Ingia kwa makini kwenye kisima, mahali ambapo mwenye ukuhani atakubatiza kwa niaba ya kila mtu. Kumbuka kukunja magoti yako na kuziba pua yako anapokushusha ndani ya maji.
5. Badilisha Nguo Zako
Baada ya kumaliza, mtu atakupa taulo. Utakaporudi kwenye chumba cha kuvalia, unaweza kuoga kwa faragha, kuvalia nguo zako kavu na kuchana nywele zako. Hakikisha unaweka nguo zako zilizolowa katika kifaa kilichowekwa na uache ufunguo wako wa kabati katika loki.
6. Shiriki katika Uthibitisho
Mwisho, mtu atakuongoza kwenye chumba ambacho utathibitishwa kwa niaba ya wale waliobatizwa.
Baadhi ya mahekalu yanaweza kufanya mambo kwa njia tofauti kidogo. Lakini bila kujali chochote, kutakuwa na watu wa kukusaidia kila hatua ya njia. Kumbuka, hekalu ni nyumba ya Bwana, na Yeye anafurahia kuwa na wewe pale!
Vielelezo na Mark Robison