“Kutembela Hekalu,” Rafiki, Novemba 2024, 18–19.
Kitu cha kuburudisha
Kutembelea Hekalu
Karibuni hekaluni!
Ndani ya hekalu, tunaweza kujifunza kuhusu mpango wa wokovu na kufanya maagano na Baba wa Mbinguni. Kuna vyumba vingi vizuri ambamo tunaweza kuhisi amani kutoka kwa Roho Mtakatifu.
Chumba cha kuunganisha ni mahali ambapo wanandoa na familia wanaunganishwa pamoja kwa muda na milele.
Chumba cha bibi harusi ni mahali wanawake wanakuwa wakijitayarisha kabla ya kuunganishwa.
Chumba cha maelekezo ni mahali unapojifunza kuhusu mpango wa wokovu na kufanya maagano matakatifu na Baba wa Mbinguni.
Chumba cha selestia hutusaidia kufikiria kuhusu vile itakavyokuwa kuishi na Baba wa Mbinguni tena. Ni mahali pa kusali, kutafakari na kusoma maandiko.
Kisima cha ubatizo ni mahali ambapo unaweza kubatizwa kwa niaba ya watu waliokufa. Maksai kumi na wawili kuzunguka kisima huwakilisha makabila kumi na mawili ya Israeli.
Orodha ya Kukagua Hekaluni
Je, unaweza kupata vitu hivi ndani ya hekalu?
-
Shada la taa zenye mapambo linaloning’inia
-
kioo
-
chombo cha maua
-
maksai wa kisima cha ubatizo
-
kioo kilichotiwa rangi