2024
Mihutasari wa Mkutano
Novemba 2024


“Mihutasari ya Mkutano,” Rafiki, Novemba 2024, 6.

Mihutasari ya Mkutano

Tiara na Maagano

Dallin H. Oaks

Rais Oaks alizungumza kuhusu mvulana na baba yake wakirusha tiara. Mvulana aliuliza kama wangekata uzi ili kuruhusu tiara kuruka juu zaidi. Baba alieleza kwamba kukata kamba kungefanya tiara kuanguka. Uzi ni kama vile maagano ambayo yanatuunganisha sisi na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Kuyashika maagano yetu hutusaidia kuja karibu na wao.

Hii inanifundisha mimi:

Dirisha la Kioo Lenye Picha

Dieter F. Uchtdorf

Mzee Uchtdorf alibatizwa miaka 75 iliyopita! Ushuhuda wake ulianza kama mvulana huko Ujerumani. Anaweza bado kukumbuka hisia takatifu alizokuwa nazo akiangalia dirisha la lenye picha ya Yesu Kristo katika kanisa lao. Roho alitoa ushahidi akilini mwake na moyoni mwake kwamba Yesu Kristo ni Mwokozi wa ulimwengu.

Hii inanifundisha mimi:

Kufokasi kwa Yesu

I. Raymond Egbo

Mzee Egbo alisimulia kuhusu timu ya mpira wa miguu ya wanaume wa Nigeria kwenye Michezo ya Olimpiki ya 1996. Hawakuwa na pesa nyingi au mafunzo bora. Lakini walifokasi kwenye lengo lao, walipuuza vivuruga mawazovingine vyote, na walishinda dhahabu! Tunapopuuza vivuruga mawazo vya ulimwengu na kufokasi kwa Yesu Kristo, tutapata pia mafanikio.

Hii inanifundisha mimi:

Kuuliza Maswali

Tracy Y. Browning

Dada Browning alisema kwamba hadi mwaka 1992, wanasayansi walidhani Pluto ndiyo mwishoi wa mfumo wetu wa jua na sayari zake. Lakini wanasayansi waliendelea kujifunza na kuuliza maswali. Sasa tunajua kwamba kuna mengi sana ya kugundua zaidi ya Pluto! Tunapokuwa na maswali, tunaweza kumgeukia Baba wa Mbinguni. Maswali ya dhati juu ya injili yanaweza kutusaidia kujifunza na kukua.

Hii inanifundisha mimi:

Ukurasa wa PDF

Vielelezo na Josh Talbot