2024
Kulima Bustani pamoja na Mama
Novemba 2024


“Kulima Bustani pamoja na Mama,” Rafiki, Novemba 2024, 30–31.

Kulima bustani na Mama

Hadithi hii ilitokea huko New Zealand.

Mama na binti ndani ya bustani

Halo, Emily! Ni vizuri kuwa nje, sivyo?

Ndiyo! Ninaweza kujaribu? Ninataka kusaidia!

Sepeto inaweza kuwa kubwa sana kwako. Kwa nini usinisaidie kung’oa magugu bustanini?

SAWA!

Mama akiwa ameshikilia gugu

Acha tuwe makini tusing’oe maua yoyote. Nitakuonyesha magugu ni yapi.

Msichana ndani ya bustani

Je, tunatakiwa kung’oa magugu yote? Yako mengi sana!

Mama akizungumza

Tunafanya kama tunataka bustani ionekane nzuri.

Msichana aliyechoka ndani ya bustani

Kutunza bustani ni vigumu.

Mama akifanya kazi kwenye vitalu vya maua

Uko sahihi. Lakini kazi bado inahitaji kufanyika.

Kwa nini tulipanda maua mengi sana? Hiyo ni kazi zaidi!

Ua la waridi

Kwa nini unafikiri Baba wa Mbinguni alitengeneza maua waridi kuwa mazuri sana?

Sijui.

Mama ameshikilia ua la waridi

Kwa sababu anataka sisi tuwe na furaha tunapoyaona.

Msichana akiwa na maua ya waridi

Ni kama wimbo ule! “Ninafurahi kwamba ninaishi katika ulimwengu huu mzuri ambao Baba wa Mbinguni aliuumba kwa ajili yangu.”

Mama na binti wakiangalia bustani

Mama: Ndio maana sijali kufanya kazi ngumu. Maua hunifanya niwe na furaha.

Emily: Yanatukumbusha juu ya upendo wa Baba wa Mbinguni!

PDF

Vielelezo na Alyssa M. Gonzalez

  • Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 228–29.