2024
Kaka wa Yaredi
Novemba 2024


“Kaka wa Yaredi,” Rafiki, Novemba 2024, 24–25.

Jifunze kuhusu Kitabu cha Mormoni

Kaka wa Yaredi

Mashua za Wayaredi

Wayaredi walijenga mashua zilizozibwa ili kusafiri kwenda nchi ya ahadi.

Matundu ya hewa kwenye mashua

Lakini kaka wa Yaredi alikuwa na swali. Ni kwa jinsi gani wangepumua ndani ya mashua? Alisali kwa ajili ya msaada, na Bwana akamwambia atoboe matundu katika mashua kwa ajili ya hewa.

Kaka wa Yaredi akitafakari

Kaka wa Yaredi alikuwa na swali lingine. Je, wangewezaje kuwa na mwanga? Wakati huu, Bwana alimwuliza kaka wa Yaredi alitaka Yeye afanye nini ili Wayaredi waweze kuwa na mwanga.

Mawe madogo kwa ajili ya mashua

Kisha kaka wa Yaredi akapata wazo. Alimwomba Bwana kugusa mawe madogo 16. Wakati Bwana alipoyagusa, yaling’aa!

Kaka wa Yaredi

Tunaweza kumwuliza Bwana maswali yetu. Yeye anataka kutusaidia kutatua matatizo yetu.

Changamoto ya Maandiko

  • Amaroni alificha wapi mabamba ya dhahabu ili Mormoni ayapate? (Mormoni 1:2–3)

  • Bwana alisimamia nini wakati alipowaambia Wayaredi wapi pa kusafiri? (Etheri 2:5)

  • Bwana aliwaleta kutoka wapi mababu wa Shule? (Etheri 7:27)

Ninaweza Kusoma Kitabu cha Mormoni!

Mawe kwa ajili ya mashua

Baada ya kusoma, paka rangi sehemu ya picha. Unaweza kusoma maandiko haya yanayoenda sambamba na usomaji wa kila wiki kutoka Njoo, Unifuate.

PDF

Vielelezo na Brooke Smart