“Habari za Mkutano,” Rafiki, Novemba 2024, 4-5
Habari za Mkutano
Nukuu za Mkutano
Kutazama Mkutano ulimwenguni kote
Ninapenda kuwasikia mitume na nabii wetu, Rais Russell M. Nelson, wakizungumza kwenye mkutano. Ninapenda kuwa na nabii mwenye umri wa miaka 100!
Luciano F., umri miaka 6, Magallanes, Chile
Rais wangu wa tawi alifanya ukurasa wa maswali na majibu ya mkutano kwa ajili ya watoto wa Msingi. Ilinisaidia kusikiliza hotuba kwenye mkutano mkuu. Ilikuwa ni ya kuburudisha sana!
Yen-Ting C., umri miaka 10, Kaunti ya Changhua, Taiwan
Mkutano mkuu ni wakati bora wa kutafuta na kupokea mwongozo binafsi wa kiungu .
Janice K., umri miaka 12, Goa, India
Kuimba katika mkutano mkuu kulinifanya nijisikie furaha, hasa nilipokuwa nikiimba kuhusu Yesu Kristo na Baba wa Mbinguni.
Annelise G., umri miaka 10, Utah, Marekani
Kwaya ya Watoto
Mamia ya watoto kutoka Utah, Marekani, waliimba katika kikao cha Jumamosi mchana. Nyimbo tatu walizoimba zilitoka katika Kitabu cha Nyimbo mpya—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani.
Kuna Mahekalu Mangapi?
Mahekalu yanajengwa kote ulimwenguni! Ni mahekalu mangapi Rais Nelson alitangaza katika mkutano huu?
-
8 katika Amerika ya Kaskazini
-
+ 1 katika Karibiani
-
+ 1 katika Amerika ya Kati
-
+ 2 katika Amerika ya Kusini
-
+ 2 katika Ulaya
-
+ 3 katika Afrika
-
= ___ mahekalu
Jumla ya Mahekalu
-
190 yanafanya kazi
-
116 yametangazwa
-
50 chini ya ujenzi
-
7 chini ya ukarabati
Sasa na Hapo Baadae
Wakati mkutano mkuu ulipoanza miaka 194 iliyopita, ni kundi dogo tu la watu waliweza kumsikia nabii ana kwa ana.
Miaka 100 iliyopita, waliweza kusikiliza mkutano kwenye redio.
Miaka 75 iliyopita, waliweza kuitazama kwenye runinga.
Miaka 25 iliyopita, waliweza kutazama au kusikiliza mtandaoni.
Leo, watu wanaweza kuangalia au kusikiliza mkutano mkuu mahali popote ulimwenguni!