2024
Mkutano Maalumu
Novemba 2024


“Mkutano Maalum,” Rafiki, Novemba 2024, 8–9.

Mkutano Maalumu

Labda kusaidia kungeweza kumfanya awe na furaha, kama Rais Nelson alivyosema.

Hadithi hii imetokea huko Indonesia.

Akina dada wakibishana juu ya mwanasesere

“Aminah, huyo ni wangu!” Indira alipiga kelele. Alimnyakua mwanasesere mbali na dada yake mdogo.

“Wasichana, ninaondoka,” Mama alisema. “Tafadhali kaeni vizuri na Baba.”

Indira alitazama juu. “Wewe unakwenda wapi?”

“Sokoni. Ninanunua chakula ili kupika kitu maalumu kesho.” Mama alipunga mkono wa kwaheri.

Mlo maalumu? Lakini kwa nini? Indira alikwenda kumtafuta Baba. “Kwa nini kesho ni maalumu?” aliuliza.

Baba akatabasamu. “Kesho tunapata kutazama mkutano mkuu! Ni maalumu kwa sababu tunapata kumsikiliza nabii na viongozi wengine wa Kanisa wakizungumza. Wanatuambia kile Baba wa Mbinguni anataka sisi tusikie.”

Wakati Mama alipofika nyumbani, alikiweka kando kile chakula. Baba alifagia sakafu.

Wazazi wakisafisha nyumba

“Indira, unaweza kumsaidia Aminah kuzipanga nguo zake kwa ajili ya kesho?” Mama aliomba.

Indira alikunja uso. “Kwa nini ninatakiwa kumsaidia?”

“Tafadhali fanya ninachoomba,” Mama alisema.

Indira aliguna. Aliburuta miguu yake na kwenda kumsaidia Aminah.

Asubuhi iliyofuata, Indira aliamka na kukutana na harufu ya utamu. Aliruka kutoka kitandani na kukimbilia jikoni. Mama alikuwa ametengeneza supu ya ng’ombe na nyama choma kwa ajili ya chakula cha mchana baadaye! Itakuwa tamu sana.

Familia ikiangalia mkutano mkuu

Punde mkutano mkuu ukaanza. Indira alikaa na familia yake kutazama kwenye runinga. Alisikiliza kwaya ikiimba. Aliwasikia watu wakizungumza kuhusu mahekalu na maandiko na Yesu Kristo.

Msemaji wa mwisho alikuwa nabii, Rais Russell M. Nelson. Alizungumza kuhusu jinsi Kanisa linavyowasaidia watu ulimwenguni kote.

Shangwe“yetu kuu huja wakati tunapowasaidia kaka zetu na dada zetu,” alisema.

Indira aliwaza kuhusu hilo. Je, kumsaidia kulimfanya awe na furaha? Aliendelea kusikiliza. Rais Nelson alisema kwamba kuishi amri kuu ya pili kunaweza kutusaidia kuwa kama Yesu Kristo.

Ulipokwisha, walikula chakula cha mchana Mama alichokipika. Indira aliendelea kufikiria kuhusu hotuba ya nabii.

Familia wakila mlo wa mchana

“Amri kuu ya pili ni nini?” aliuliza.

“Mpende jirani yako kama nafsi yako,” Baba alisema.

Indira alifikiria kuhusu watu waliosaidiwa na Kanisa ulimwenguni kote. “Ninawezaje kusaidia ikiwa majirani zangu wanaishi mbali sana?”

“Jirani zako ni kila mtu aliye karibu nawe,” Mama alisema. “Kama wanafamilia wako.”

Indira alitazama chini. Hakuwa mwema sana kwa familia yake wakati mwingine.

Lakini labda kuwasaidia kungeweza kumfurahisha, kama Rais Nelson alivyosema. Ilikuwa njia mojawapo ambayo angeweza kumfuata Yesu. Alitaka kujaribu!

Kwa wiki nzima, Indira alijaribu kuwa mwema zaidi kwa familia yake. Alicheza na Amirah. Alishiriki wanasesere wake. Alifanya kile Mama na Baba walichomwambia bila kulalamika. Wakati Indira alipoisaidia familia yake, walikuwa na furaha. Na hilo lilimfanya awe na furaha pia.

Akina dada wakicheza pamoja

Nabii alikuwa sahihi. Kuwasaidia wengine kulimletea shangwe!

Msichana ikitembea nje
PDF

Vielelezo na Judi Abbot

  1. Amri Kuu ya Pili,” Liahona, Nov. 2019, 100.

  2. Ona Mathayo 22:37–39.