“Shughuli za Njoo, Unifuate ,” Rafiki, Novemba 2024, 28–29.
Shughuli za Njoo, Unifuate
Kwa ajili ya jioni ya nyumbani, au kujifunza maandiko—au kwa ajili ya burudani tu!
Oktoba 28–Novemba 3
Pendaneni
Kwa ajili ya Mormoni 1–6
Mormoni aliwapenda Wanefi (ona Mormoni 3:12). Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wametuomba tuwapende wengine pia. Simameni katika duara na fungeni macho yenu. Hesabu hadi tatu, kisha fungueni macho yenu na umwangalie mtu fulani. Ikiwa unaangaliana nao machoni, sema kitu fulani unachopenda kuhusu kila mmoja na uondoke kwenye duara. Endelea kwenda mpaka pale mtu mmoja abakie! Kisha kila mtu anasema kitu fulani wanachokipenda kuhusu mtu huyo.
Novemba 4–10
Sanaa ya Muujiza
Kwa ajili ya Mormoni 7–9
Tunapomfuata Yesu Kristo, Baba wa Mbinguni anaweza kutubariki kwa miujiza. Soma Mormoni 8:24 na uchore mojawapo ya miujiza iliyoelezwa katika mstari huo. Wakati ukichora, zungumza kuhusu miujiza gani Baba wa Mbinguni ameifanya kwa ajili ya familia yako.
Novemba 11–17
Kuchora Miamba
Kwa ajili ya Etheri 1–5.
Kaka wa Yaredi alimwomba Bwana kugusa mawe ili mashua zake ziweze kuwa na mwanga (ona Etheri 3). Kusanya mawe kutoka nje au kata duara kutoka vipande vya karatasi. Kwenye mawe yako au karatasi, andika, chora au paka rangi vitu ambavyo unaweza kufanya ili kuleta nuru na upendo kwa wengine.
Novemba 18–24
Nyimbo za Shukrani
Kwa ajili ya Etheri 6–11
Walipokuwa wakisafiri kuvuka bahari, kaka wa Yaredi na familia yake waliimba sifa kwa Bwana kumshukuru kwa kuwasaidia (ona Etheri 6:9). Unaweza kuimba kumshukuru Bwana pia! Chagua wimbo uupendao kutoka kwenye Kitabu cha Nyimbo za Watoto au tovuti ya Kanisa na muimbe kwa pamoja. Unawezaje kumwonyesha Baba wa Mbinguni kuwa una shukrani?
Vielelezo na Katy Dockrill