2024
Kuunganishwa Hekaluni ni Nini?
Novemba 2024


“Kuunganishwa Hekaluni ni nini? Rafiki, Novemba 2024, 22.

Kadi za Mahekalu

Kuunganishwa Hekaluni ni nini?

Kuunganishwa hekaluni ni ibada ambayo huunganisha familia pamoja milele. Hii inamaanisha kwamba kama tutashika maagano yetu na kumtii Mungu, tutaishi na familia yetu tena baada ya kufa kwetu. Manabii wameahidi kwamba kwa sababu ya Yesu Kristo, familia zinaweza kuwa za milele.

Hekalu la Nairobi Kenya

  • Hili ni hekalu la tisa lililojengwa Afrika na la kwanza nchini Kenya.

  • Waumini wa Kanisa kote Afrika Mashariki watakuja kwenye hekalu hili.

  • Mnamo mwaka 1998 Rais Hinckley alisema hekalu litajengwa siku moja nchini Kenya. Hekalu hili lilitangazwa miaka 19 baadaye.

Hekalu la Papeete Tahiti

  • Baada ya hekalu hili kurekebishwa mwaka 2006, maelfu ya watu walifanya tukio la kitamaduni kusherehekea kuwekwa wakfu upya.

  • Lina paa maridadi la bluu.

  • Kabla ya hekalu hili kujengwa mwaka 1983, hekalu la karibu sana na Tahiti lilikuwa New Zealand.

PDF

Vielelezo na Rachel Erickson