2024
Kumfuata Yesu huko Kenya
Novemba 2024


“Kumfuata Yesu huko Kenya,” Rafiki, Novemba. 2024, 10–11.

Kumfuata Yesu huko Kenya

Kutana na Martin!

Martin kutoka Kenya

Jinsi Martin Anavyomfuata Yesu

Martin anamfuata Yesu kwa kujifunza kumhusu Yeye. Wakati Martin alipokutana na wamisionari, walimpa kijitabu kuhusu Yesu Kristo. Martin ana ulemavu wa kuona, hivyo hakuweza kusoma maneno madogo. Lakini bado alitaka kujifunza zaidi.

Wamisionari walimpa Martin nakala ya Kitabu cha Mormoni kwa breli. Breli ni aina ya lugha iliyoandikwa kwa ajili ya watu ambao ni vipofu au wenye ulemavu wa kuona.

Martin akisoma kwa breli

Martin alichagua kubatizwa pamoja na baba yake. “Ninashukuru kwa ajili ya Kanisa la Yesu Kristo,” Martin anasema. “Mimi najua ni la kweli.”

Kuhusu Martin

Martin mbele ya ramani

Umri: miaka 10

Kutoka Nairobi, Kenya

Lugha: Kiingereza, Kiswahili,

Malengo: 1) Kueneza nuru ya Yesu Kristo. 2) Kutumikia misheni. 3) Kuwa mwanasheria.

Mambo ayapendayo : Kucheza chesi, kumsaidia baba yake na biashara yake ya kutengeneza nguo

Familia: Martin, Baba, kaka mkubwa

Mambo Ayapendayo Martin

Hadithi ya Kitabu cha Mormoni: Wakati mizigo ya Wanefi ilipofanywa kuwa miepesi (ona Mosia 24)

Likizo: Siku ya Mashujaa

Matunda: Mapeazi

Rangi: Bluu

Wimbo wa Watoto:I Am a Child of God” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 2–3)

PDF ya hadithi