2024
Je, Ninatakiwa Kuwa Mkamilifu?
Novemba 2024


“Je, Ninatakiwa Kuwa Mkamilifu?” Rafiki Novemba 2024, 36–37.

Je, Ninatakiwa Kuwa Mkamilifu?

Henry alitaka kwenda hekaluni, lakini alihisi kama alifanya makosa mengi sana.

Hadithi hii ilitokea huko Aruba.

Henry taratibu aliingia katika chumba cha Darasa la Watoto. Miguu yake ilionekana kuwa mizito alipofika kwenye kiti chake.

Mwalimu wake, Kaka Rass, alitabasamu kwake. “Je, uko tayari kuzungumza kuhusu mahekalu?” aliuliza.

“Ndio,” Henry alijibu.

Kwa nini nilisema hivyo? Henry alifikiria alipokuwa ameketi chini. Yeye hakuhisi kuwa tayari. Kabisa.

Darasa la Watoto la Henry walikuwa wakijifunza wimbo “I Love to See the Temple.” Darasa lake walikuwa wameombwa kuzungumza kuhusu kwenda hekaluni.

Lakini Henry alihisi huzuni. Alitaka kwenda hekaluni atakapokuwa mkubwa vya kutosha, lakini alihisi kama amefanya makosa mengi.

Mmoja baada ya mwingine, marafiki wa Henry walisimama. Walikuwa na furaha na wenye shauku walipokuwa wakizungumza kuhusu kwenda hekaluni siku moja. Henry alihisi vibaya zaidi na zaidi.

Kisha ukawa wakati wa kuimba. Henry aliimba pamoja na watoto wengine wa Darasa la Watoto: “I’ll prepare myself while I am young; this is my sacred duty.”

Ninawezaje kujiandaa kwenda hekaluni wakati ninafanya makosa mengi? Henry alifikiri. Alijilaza chini kwenye kiti chake.

Wakati wimbo ulipomalizika, Kaka Rass alimwinamia. “Uko sawa?” alimwuliza Henry.

Mvulana akifikiria kuhusu hekalu

Henry alitazama chini kwenye mikono yake. Kisha akasema kwa upole, “Nataka kwenda hekaluni, lakini ninaogopa kwamba sistahili.” Alivuta pumzi ndefu. “Siyo siku zote naelewana na familia yangu. Ninasahau kufanya kazi zangu za nyumbani. Ninafanya makosa mengi sana. Je, ninahitaji kuwa mkamilifu?”

Kaka Rass alitabasamu kwa upole. “Kuwa mwenye kustahili kwenda hekaluni haimaanishi kwamba unatakiwa kuwa mkamilifu. Tunaweza kuwa wastahiki kwa kumtumaini Yesu Kristo na kujaribu kwa dhati kushika amri. Sote tunafanya makosa, lakini tunaweza kutubu na kuwa wasafi tena.”

Henry alikaa wima kidogo.

“Nina hakika Baba wa Mbinguni anajivunia wewe kwa kujaribu kuwa mwema,” alisema Kaka Rass.

Henry alifikiria kuhusu baadhi ya mambo mazuri aliyokuwa ameyafanya wiki hiyo. Alipika chakula cha jioni pamoja na Mama, alimsaidia dada yake kazi ya nyumbani, na kumsalimia mvulana mpya shuleni.

Uzito wa wasiwasi wa Henry ulianza kutoweka. Alijua Roho Mtakatifu alikuwa akimsaidia kuhisi amani.

Mvulana akifurahi kwenda hekaluni.

Ilipofika zamu ya Henry kushiriki, alitabasamu na kusimama. “Ninataka kuendelea kutubu na kuwa zaidi kama Yesu Kristo ili kwamba siku moja niweze kuingia hekaluni,” alisema.

Henry alihisi furaha alipokuwa ameketi chini. Siku moja, angeweza kufanya maagano matakatifu na Mungu ndani ya hekalu. Alitaka kujaribu kadiri awezavyo kujiandaa!

PDF

Vielelezo na Gail Armstrong

  • Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 95