2024
Kuunganishwa kwa Maagano
Novemba 2024


“Kuunganishwa kwa Maagano,” Rafiki, Novemba 2023, 21.

Kitu cha kuburudisha

Kuunganishwa kwa Maagano

Yesu Kristo

Maagano yanatuunganisha sisi kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Kwa kushika maagano yetu, tunaweza kupokea msaada na nguvu za mbinguni. Rais Nelson alifundisha, “Mara tu mimi na wewe tunapokuwa tumefanya agano na Mungu, uhusiano wetu na Yeye unakuwa wa karibu zaidi. … Kwa sababu ya agano letu na [Yeye], Yeye kamwe hatachoka katika juhudi Zake za kutusaidia.”

Tengeneza mnyororo wa viungo ili kukukumbusha juu ya agano lako la ubatizo! Kisha uning’inize mahali utakapouona.

Sanaa ya mnyororo wa karatasi
  1. Kata vipande sita vya karatasi karibu inchi 1 (sentimita 2.5) kwa upana na inchi 8 (sentimita 20) urefu.

  2. Kwenye kila kipande, andika mojawapo ya njia unazoweza kushika agano lako la ubatizo. (Orodha iliyopo hapo chini inaweza kusaidia.)

  3. Chukua kipande cha kwanza na unganisha ncha zake pamoja ili kutengeneza duara. Kisha ingiza kipande kinachofuata kupitia duara na unganisha ncha hizo. Endelea kuongeza viungo mpaka uwe na mnyororo!

PDF

Kielelezo na Katy Dockrill