“Yesu Kristo Atakuja Tena,” Rafiki, Novemba 2024, 2–3.
Ujumbe wa Mkutano kutoka kwa Nabii
Yesu Kristo Atakuja Tena
Imetoholewa kutoka katika “Bwana Yesu Kristo Atakuja Tena,” Liahona, Nov. 2024, 121–22.
Mwokozi alitoa ahadi hii kwako: “Nitakuwa mkono wenu wa kuume na wa kushoto, na Roho wangu atakuwa mioyoni mwenu, na malaika zangu watawazingira, ili kuwabeba juu” (Mafundisho na Maagano 84:88).
Yesu Kristo alijichukulia juu Yake dhambi zako, maumivu yako, na huzuni yako ya moyo. Atakusamehe unapotubu. Atakubariki na kile unachohitaji.
Leo ninawaomba msaidie kuuandaa ulimwengu kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Bwana. Ninawasihi mzungumze kuhusu Kristo, mshuhudie kuhusu Kristo, muwe na imani katika Kristo, na mfurahie katika Kristo! Hii ni siri ya maisha ya furaha.
Kilicho bora bado huja tunapogeuza mioyo yetu na maisha yetu kwa Yesu Kristo.
Tayari Wakati Atakapokuja Tena
Rais Nelson alitualika kujiandaa kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Yesu Kristo. Chora picha ya kile utakachofanya ili kujiandaa. Tafuta hapa chini kwa ajili ya baadhi ya mawazo kutoka kwenye hotuba ya Rais Nelson!
Fanya na shika maagano
Saidia kuwaleta wengine kwa Kristo.
Jiandae kwenda hekaluni
Jifunze kuhusu Yesu Kristo na Upatanisho Wake