“Salamu kutoka Kenya!” Rafiki Novemba 2024, 12–13.
Salamu kutoka Kenya!
Jifunze kuhusu watoto wa Baba wa Mbinguni ulimwenguni kote.
Kenya iko Afrika Mashariki. Takribani watu milioni 50 wanaishi huko!
Lugha
Kenya ina lugha rasmi mbili: Kiswahili na Kiingereza. Dazani ya lugha zingine pia huzungumzwa huko.
Kutembelea Kenya
Mnamo Mei 2022, Mzee Ronald A. Rasband alitembelea eneo la ujenzi wa Hekalu la Nairobi Kenya. Alisema ilikuwa moja ya nyakati alizozipenda sana wakati wa safari yake ya kwenda Kenya.
Makundi ya Flamingo
Wakati Ziwa Nakuru lina mwani mwingi, maelfu ya flamingo huja kuula. Idadi ya flamingo inaweza kufanya ziwa zima lionekane waridi!
Wakimbiaji wa Ajabu
Kenya ni nyumbani kwa wengi wa wakimbiaji bora wa umbali mrefu ulimwenguni. Wameshinda medali 106 kutokana na matukio ya mbio katika Olimpiki.
Vielelezo na Ruth Hammond