2024
Mormoni na Mabamba ya Dhahabu
Novemba 2024


“Mormoni na Mabamba ya Dhahabu,” Rafiki, Novemba 2024, 26–27.

Hadithi za Maandiko

Mormoni na Mabamba ya Dhahabu

Mormoni akijifunza kuhusu mabamba

Vielelezo na Andrew Bosley

Mormoni alikuwa nabii. Alipokuwa na umri wa miaka 10, kiongozi aliyeitwa Amaroni alimwambia akumbuke kilichotokea kwa watu wake ili aweze kukiandika kwenye mabamba ya dhahabu baadaye. Mabamba ni kitu ambacho juu yake manabii wa Kinefi walikuwa wakiandika.

Kujificha na kuyatafuta mabamba

Amaroni alificha mabamba kwa sababu watu wengi walikuwa wanakuwa waovu. Alimwambia Mormoni mahali pa kuyapata. Wakati Mormoni alipokuwa mkubwa, aliyachukua yale mabamba ya dhahabu. Aliyahifadhi na kuandika kuhusu watu wake.

Mormoni akiandika kwenye mabamba

Watu bado walikuwa waovu, lakini Mormoni alijaribu kuwafundisha. Aliandika pia kuhusu Mwokozi kwenye mabamba hayo. Kwa sababu ya Mormoni, tunaweza kusoma maneno ya manabii katika Kitabu cha Mormoni leo.

Watoto wakisoma Kitabu cha Mormoni

Japokuwa Mormoni alikuwa kijana, Bwana alimwamini. Unaweza kumfuata Bwana wakati ukiwa mdogo pia!