2025
Dondoo za Kitabu cha Maelezo
Machi 2025


Dondoo za Kitabu cha Maelezo

Kazi ya Mungu ya Wokovu na Kuinuliwa

Tunapokuja kwa Kristo na kuwasaidia wengine kufanya vivyo hivyo, tunashiriki katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. Kazi hii inaongozwa na amri kuu mbili ya kumpenda Mungu na kuwapenda jirani zetu (ona Mathayo 22:37–39).

Kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa inafokasi kwenye majukumu manne matakatifu yaliyoainishwa. Haya yamebainishwa hapa chini.

1. Kuishi Injili ya Yesu Kristo

  • Kufanyia kazi imani katika Kristo, kutubu kila siku, kufanya maagano na Mungu pale tunapopokea ibada za wokovu na kuinuliwa na kuvumilia hadi mwisho kwa kutii maagano hayo.

  • Kujifunza na kufundisha injili ya Yesu Kristo nyumbani na kanisani.

  • Kuwa wenye kujitegemea katika kukidhi mahitaji yetu wenyewe na ya familia zetu, kiroho na kimwili.

2. Kuwajali Wenye Mahitaji

  • Kuwatumikia na kuwahudumia watu binafsi, familia na jumuiya.

  • Kushiriki rasilimali, ikiwa ni pamoja na msaada wa Kanisa, kwa wenye mahitaji.

  • Kuwasaidia wengine wawe wenye kujitegemea.

3. Kuwaalika Wote Waipokee Injili

  • Kushiriki katika kazi ya umisionari na kutumikia kama wamisionari.

  • Kuwasaidia waumini wapya na wanaorudi kupiga hatua kwenye njia ya agano.

4. Kuziunganisha Familia kwa ajili ya Milele

  • Kufanya maagano pale tunapopokea ibada zetu wenyewe.

  • Kuwatambua mababu zetu waliofariki na kufanya ibada kwa ajili yao ndani ya hekalu ili waweze kufanya maagano na Mungu.

Kwenda hekaluni mara kwa mara, pale inapowezekana, ili kumwabudu Mungu na kufanya ibada kwa ajili ya watoto Wake.