“Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,” Liahona, Machi 2025.
Kanisa Liko Hapa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Waongofu wa kwanza katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo walibatizwa nje ya nchi kabla ya kurudi katika nchi yao ya nyumbani na kushiriki imani yao na wengine. Wakati wamisionari walipowasili DRC mnamo 1986, tayari kulikuwa na makundi ya waongofu wakikutana kila wiki. Kigingi cha kwanza kiliundwa mwaka 1996, na hekalu la kwanza nchini liliwekwa wakfu mwaka 2019. Leo, Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo lina:
-
Waumini 115,000 (kwa makadirio)
-
Vigingi 27, kata na matawi 289, misheni 5
-
Hekalu 1 (Kinshasa) na 3 yalitangazwa (Lubumbashi, Kananga, na Mbuji-Mayi)
Shukrani kwa ajili ya Mpango wa Wokovu
Wakati John Lwamba kutoka Lubumbashi alipokuwa akihudumu misheni, kaka yake mkubwa alifariki. Anasema, “Ilikuwa vigumu kidogo kwangu kukubali kwa sababu alikuwa mtu wa kwanza katika familia yangu kufariki. Kwa usaidizi wa rais wangu wa misheni na maandiko, niliweza kuikubali, na tangu siku hiyo, uzoefu huu umenileta karibu na Mwokozi. Ninajua kwamba alipofufuka, wanafamilia wangu wote ambao wamefariki watafufuka tena.”