“Mungu Alizungumza na Watakatifu wa Mwanzo—Je, Anazungumza Nami?,” Liahona, Machi 2024.
Vijana Wakubwa
Mungu Alizungumza na Watakatifu wa Mwanzo—Je, Anazungumza Nami?
Alizungumza nao. Atazungumza nasi. Unapaswa tu kumsikiliza Yeye.”
Nguzo ya mwanga Sauti kutoka mbinguni Ufunuo kutoka kwa Mungu. Kuna hadithi nyingi za vijana wakubwa kama Joseph Smith na wengine katika Mafundisho na Maagano ambao walimwomba Mungu msaada na mwongozo. Wakati kupokea ufunuo kutoka kwa Mungu ni uzoefu binafsi, mchakato huo umerekodiwa mara kwa mara katika maandiko.
Hata kama hatuwezi kuchangamana kila siku na nabii au kupokea ufunuo kwa ajili ya Kanisa, Mungu anaweza kuzungumza nasi katika njia sawa na zile alizofanya miaka 200 iliyopita. Watakatifu hawa walipokea jumbe binafsi kutoka kwa Mungu—na sisi pia tunaweza.
Sala ya Unyenyekevu ya Joseph
Ilianza na swali. Na ikawa kile Mzee Alexander Dushku wa Sabini alichokielezea kama “mpasuko ulijawa nuru na ukweli.” Sala ya Joseph Smith ya unyenyekevu ilisababisha matembezi ya Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo (ona Joseph Smith—Historia ya 1:14–17). Cha kushangaza jinsi itakavyokuwa kuongea na Mungu ana kwa ana, uzoefu huu ni wa nadra na mtakatifu.
Wakati siyo sisi sote tutakuwa na fursa sawa na ile iliyofanyika kwa Joseph, “sisi pia tunaweza kuwa na nguzo yetu wenyewe ya mwanga—mwale mmoja kwa wakati.” Tunapouliza swali na kupiga magoti katika sala ya unyenyekevu, tutapokea jibu kutoka kwa Mungu kupitia Roho Mtakatifu.
Picha ya kisima cha ubatizo katika Hekalu la Ogden Utah
Nguvu ya Hekalu
Watakatifu huko Kirtland, Ohio, walijitolea dhabihu ya muda, pesa, na kufanya kazi kujenga nyumba ya Bwana. Wakati wa kuweka wakfu Hekalu la Kirtland, Joseph Smith aliomba kwamba Mungu angewabariki Watakatifu hawa waaminifu kwa nguvu walipoingia na kuabudu (ona Mafundisho na Maagano 109:13). Hekalu hili lilikuwa liwe “nyumba ya sala, nyumba ya kufunga, nyumba ya imani, nyumba ya utukufu na ya Mungu” (Mafundisho na Maagano 109:16).
Katika siku za mwisho, tunabarikiwa na mahekalu kote ulimwenguni. Tumeahidiwa kwamba tutapokea ufunuo tunapohudhuria hekaluni. Rais Russell M. Nelson hivi karibuni alisema kwamba “katika hekalu tunaweza ‘kupokea utimilifu wa Roho Mtakatifu’ [Mafundisho na Maagano 109:15]. Fikiria kwamba hiyo ahadi inamaanisha nini kwa maana ya kuwa mbingu kufunguliwa kwa kila mmoja aliye mtafutaji wa dhati wa ukweli wa milele.”
Swali la Hyrum kwa Nabii
Je, umewahi kujiuliza ingekuwaje kumuomba nabii azungumze na Mungu kwa ajili yako? Hyrum, kaka wa Nabii Joseph, alifanya hivyo tu. Alipokea ushauri huu kutoka kwa Bwana kupitia Joseph: “Tazama wewe ni Hyrum, mwanangu; tafuta ufalme wa Mungu, na mambo yote yataongezwa kulingana na yale yaliyo ya haki” (Mafundisho na Maagano 11:23).
Wakati mwingine, mwongozo huja kupitia watu wengine. Rais Russell M. Nelson alitushauri “tutafute mwongozo kutoka kwa sauti unazoweza kuamini—kutoka kwa manabii, waonaji, na wafunuzi na kutokana na minong’ono ya Roho Mtakatifu.” Kwa vile hatuwezi sote kumuuliza nabii maswali yetu moja kwa moja, bado tunaweza kupokea majibu ya maswali yetu binafsi.
Picha ya Oliver Cowdery, na Lewis A. Ramsey
Mafunzo ya Imani ya Oliver
Oliver Cowdery alikuwa msaada mkubwa kwa Joseph wakati wa kutafsiri Kitabu cha Mormoni. Lakini mwaka 1829, alihisi kuchanganyikiwa. Kwa nini yeye hakuweza kutafsiri? Bwana alimpa Oliver baadhi ya ushauri mahususi kuhusu jinsi ya kupata jibu la swali lake—ushauri ambao bado unatumika kwetu leo.
Tunapokuwa na swali, tunahimizwa kujifunza, kuwa na imani, na kutegemea misukumo (ona Mafundisho na Maagano 9:6–9). Misukumo yetu inaweza kuja katika hali ya hisia, hisia za upendo, au amani ya akili. Kama Mzee Mathias Held wa Sabini alivyosema, “Wakati [mantiki ya kufikiria na mwongozo wa kiungu wa Roho Mtakatifu] kisha hujumuishwa katika nafsi zetu, picha moja kamili inaonyesha uhalisia wa mambo kama yalivyo kikweli.”
Picha na Craig Alan Shelley
Baraka za Patriaki za Familia ya Smith
Baraka za patriaki zimekuwa sehemu ya Kanisa tangu nyakati za Agano la Kale (ona Mwanzo 48). Wakati Kanisa lilipoanzishwa katika siku za mwisho, Mungu alimwambia Joseph kumwita baba yake, Joseph Smith Mkubwa., kama patriaki mwaka 1834. Siku tatu baadaye, familia ya Smith ilikusanyika ili Joseph Smith Mkubwa aweze kutoa baraka ya patriaki kwa kila mmoja wa watoto wake na wake zao. Baraka hizi zilitoa ushauri na faraja kwa ajili ya maisha yao.
Kwa ziada ya tamko la ukoo, baraka ya patriaki “ni maandiko binafsi kwako.” “Mtu anayepokea baraka ya patriaki anapaswa kuthamini maneno yake, kuyatafakari na kuishi kwa kustahili kupokea baraka zilizoahidiwa katika maisha haya na umilele.”
Picha ya Emma Smith, na Lee Green Richards
Maelekezo Binafsi ya Emma kutoka kwa Mungu
Kama mke kwa nabii, Emma Smith mara nyingi alipambana na majaribu na migogoro ambayo familia yake iliombwa kuvumilia. Katika Mafundisho na Maagano 25, tunaweza kusoma maneno ya Baba wa Mbinguni ya faraja na nguvu kwa Emma.
Tunapotafuta jumbe zetu wenyewe za faraja kutoka kwa Baba wa Mbinguni, tunaweza kuomba baraka za ukuhani. Kama Rais James E. Faust (1920–2007), Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza, alivyofundisha: “Baraka za ukuhani zinaweza kutusaidia katika maamuzi madogo na makubwa ya maisha yetu. Kama, kupitia baraka zetu za ukuhani, tungeweza kuona sehemu ndogo tu ya mtu ambaye Mungu anatukusudia tuwe, tungepoteza hofu yetu na kamwe tusiwe na shaka tena.”
picha yaJ oseph F.Smith, na Albert E. Salzbrenner
Kujifunza Maandiko kwa Joseph F. Smith
Wakati magonjwa, vita, na vifo vilipoangamiza ulimwengu mwaka 1918, nabii Joseph F. Smith aligeukia maandiko ili kupata majibu. Baada ya kujifunza maneno ya Petro katika Agano Jipya, alianza kufikiria na kutafakari. Alisombwa mbali katika ono kwa ajili ya Kanisa ambapo alimwona Mwokozi akianzisha kazi ya umisionari katika ulimwengu wa roho. (Ona Mafundisho na Maagano 138.)
Kama Mzee Robert D. Hales (1932–2017) wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alivyofundisha: “Tunapotaka kuzungumza na Mungu, sisi tunasali. Na wakati tunapotaka Yeye azungumze nasi, tunayapekua maandiko.” Maandiko ni maneno ya Mungu yaliyohifadhiwa katika maandishi, na katika zama zetu za kidijitali, hayajawahi kupatikana kwetu kama hivi leo. Tunaposoma na kutafakari maandiko, tutapata msaada kutoka mbinguni ambao tunauhitaji.
Picha na John McKinney
Juhudi za Makusudi za Kumsikiliza Yeye
Rais Russell M. Nelson alifundisha: “Tunapotafuta kuwa wafuasi wa Yesu Kristo, jitihada zetu za kumsikiliza Yeye zinatakiwa ziwe za makusudi zaidi. Inachukua juhudi za hiari na za dhati kujaza maisha yetu ya kila siku kwa maneno Yake, mafundisho Yake na kweli Zake.” Kama vile Watakatifu wa mwanzo, tunaweza kupokea jumbe kutoka kwa Mungu ambazo ni za kibinafsi na halisi.
Mungu alizungumza nao. Atazungumza nasi. Unapaswa tu kumsikiliza Yeye.”