“Ni nani Aliyejaza Kisima?” Liahona, Machi 2025.
Sauti za Watakatifu wa Siku za Mwisho
Nani Alijaza Kisima?
Bila maji yanayopatikana kutoka mjini, ni kwa jinsi gani tulipaswa kumbatiza Megan?
Kielelezo na David Miles
Baada ya kukosa basi jijini Nairobi, Kenya, mimi na mwenzangu tuliamua kushiriki injili na kila mmoja tuliyemwona wakati tukisubiri basi lingine kwenda eneo letu. Tulizungumza na zaidi ya watu 400.
Mmoja wao alikuwa Benard, ambaye alifanya kazi ya ujenzi jirani na tulipokuwa. Tulimpatia Kitabu cha Mormoni na kumpa changamoto ya kukisoma kila siku na kumuuliza Mungu kama kilikuwa cha kweli.
Miezi minne baadaye, nilihamishiwa Nairobi. Katika mkutano wangu wa kwanza wa sakramenti huko, nilimwona Benard. Tangu hapo alikuwa amebatizwa na kutawazwa katika Ukuhani wa Haruni.
Benard kwa msisimko alitualika tutembelee nyumbani kwake na kumfundisha mke wake, Megan. Tulipokutana na Megan, tulipigwa na butwaa kwa imani yake kuu. Aliposali ili kujua kama ujumbe wetu ulikuwa wa kweli, Mungu alijibu sala yake.
Tulimwalika Megan kubatizwa Jumapili iliyofuata. Wiki hiyo, hata hivyo, mji wa Nairobi ulitangaza kwamba maji yangekatwa kwa siku 10! Baada ya mahojiano ya Megan ya ubatizo Jumamosi, mimi na mwenzangu tuliomba kwamba ubatizo wake ungeweza kusonga mbele siku iliyofuata.
Tulifunga, tulishauriana na viongozi wetu, na kujaribu njia tofauti za kupata maji—yote bila mafanikio. Jioni hiyo tulijiandaa kwa ajili ya ubatizo hata hivyo. Kisha tukapiga magoti na kusali tena. Tulihisi msukumo wa kuchomeka mwisho mmoja wa mpira kwenye bomba kavu la jikoni na kuweka mwisho mwingine katika kisima cha ubatizo. Tulisema sala nyinginei, tukafunga jengo, na tukaondoka kwenda nyumbani.
Asubuhi iliyofuata tulipokwenda kwenye jumba la mikutano, kwa mshangao wetu kisima kilikuwa kimejaa maji! Tuliangalia bomba la jikoni, lakini bado hakuna maji yaliyotoka. Hakuna yeyote kutoka tawini aliyekuwa na kidokezo kuhusu jinsi kisima kilivyojazwa.
Megan alibatizwa siku hiyo. Kata yote ilikuja kushuhudia ubatizo wake na kumkaribisha katika Kanisa. Bomba lilibaki kavu, lakini macho ya kila mtu yalikuwa yamelowa kwa machozi ya shukrani.
Rais Russell M. Nelson amefundisha, “Bwana atakubariki wewe kwa miujiza kama unamwamini Yeye, ‘pasipo shaka yo yote’ [Mormoni 9:21]. Fanya kazi ya kiroho ili kutafuta miujiza.” Ninajua kwamba kwa sababu mimi na mwenzangu tulifanya kazi ya kimwili na kiroho—kusali, kujaribu chaguzi tofauti, na kufuata misukumo ya kiroho—tuliona muujiza kutoka kwa Bwana.