2025
Ni kwa Jinsi Gani Maagano Yetu Hutusaidia Kuvuta Nguvu za Mungu?
Machi 2025


“Ni kwa Jinsi Gani Maagano Yetu Hutusaidia Kuvuta Nguvu za Mungu?,” Liahona, Machi 2025.

Wanawake wa Agano

Ni kwa Jinsi Gani Maagano Yetu Hutusaidia Kuvuta Nguvu za Mungu?

Kama wanawake wa agano, nguvu za Mungu hutubadilisha, hutuimarisha, na hutupatia kujiamini.

mwanamke ufukoni pamoja na mabinti zake wadogo

Picha na Connor Johnson

Kila mmoja wetu ana fursa ya kufanya maagano matakatifu na huyu Mungu wa mbinguni. Tunafanya maagano haya wakati tunapopokea ibada za ukuhani. Tunaposhika maagano haya, Yeye hutubariki na nguvu Yake

Kumbuka pamoja nami maelekezo ya kinabii wa Rais Russell M. Nelson kuhusu jinsi ya kupata nguvu kutoka kwa Mungu: “Kila mwanaume na kila mwanamke anayeshiriki katika ibada za ukuhani na anayefanya na kushika maagano na Mungu ana fursa ya moja kwa moja kwenye nguvu za Mungu.” Upatikanaji huu wa moja kwa moja wa nguvu za Mungu ni zawadi ambayo kwa ukarimu anashiriki na watoto Wake.

Nguvu hii inafanya nini, ambacho kinatiririka kutokana na kushika maagano tunayofanya kupitia ibada za ukuhani, inayoonekana katika maisha yako ya siku hadi siku? Ni kwa jinsi gani mwanamke wa agano anavyovuta nguvu hii takatifu?

Natumaini mfano binafsi utakusaidia unapofanya kazi ya kiroho ya kujifunza wewe mwenyewe kile inachomaanisha kuvikwa nguvu ya Mungu.

Siku moja nilipokea ujumbe mfupi kutoka kwa binti mkwe wangu Amy: “Sema sala kwa ajili ya Dottie.”

Mjukuu wangu Dottie hakuwa amelala usiku jana yake. Amy alikuwa macho usiku mzima pamoja naye na kusema kwamba Dottie alikuwa na homa. Amy alimpa dawa fulani, lakini Dottie alikuwa bado na joto na asiye na utulivu. Na mwana wangu Connor alikuwa akisafiri kwenda kazini na hakupanga kuwa nyumbani kwa siku nyingine mbili.

Asubuhi hatimaye ilipofika, Amy alipata midomo ya Dottie ikiwa ya bluu. Mikono yake vivyo hivyo ilikuwa ya bluu na baridi ukiigusa. Amy mara moja alipata msukumo, “Mpeleke Dottie kwa daktari wa watoto.” Alitii ushawishi huo, alipiga simu kwenye ofisi ya daktani wa watoto, na alihakikishiwa kuwa wangemwingiza Dottie moja kwa moja kwa daktari.

Kwa bahati nzuri, ofisi ya daktari wa watoto iko ghambo ya barabara tu kutoka nyumba ya mama yangu. Amy alihisi msukumo wa kuendesha gari kupitia nyumbani kwa mama yangu. Mama yangu alikuwa akifanya kazi katika uga wake na alifurahi kumpeleka dada wa Dottie mwenye umri wa miaka minne, Goldie, wakati Amy alipompeleka Dottie kwa daktari wa watoto. Ilikuwa ni jibu kwa wasiwasi wa Amy kuhusu kuhitaji wa kumfuatilia Goldie na kumwangalia Dottie kwa wakati mmoja.

Daktari wa watoto aligundua kwamba Dottie alikuwa na nimonia, yawezekana ilitokana na kutamani maji ya kuoga mara kwa mara siku chache zilizopita. Dottie alitibiwa na antibiotiki na alitumia siku nzima katika mikono ya mama yake, aliinuliwa kufungua njia zake za hewa na kushusha pumzi yake.

Nilijitolea kuchukua chakula cha jioni nikiwa njiani kuelekea nyumbani. Na Amy akaniruhusu, kwa ajili ya hayo niliyokuwa na shukrani. Nilishangaa jinsi Amy alivyoweza baada ya usiku usio na usingizi, msongo wa mawazo wa kuwa na mtoto mchanga mgonjwa, na haja ya kuwangalia Goldie.

Niliingia nyumbani mwao na mfuko wa chakula cha kubeba mkononi na kumkuta Amy na wasichana wakiwa na amani. Kulikuwa na machozi usoni mwa Amy na nuru katika uso wake. Alikuwa mtulivu, hata kukabili usiku mwingine pekee yake na Dottie mgonjwa. Hakuwa anaogopa. Alikuwa jasiri. Ilikuwa ni amani ambayo ilishinda uelewa. Nilitaka tu kukaa kwa muda na kuloweka ndani.

Amy anajitahidi kushika maagano yake na Mungu na alibarikiwa kwa nguvu Yake ya kuimarisha. Roho alikuwa amemsukuma kuchukua hatua alizofanya kumtunza Dottie. Na nguvu za Bwana ziliongeza uwezo wake wa kushughulikia mahitaji ya familia yake kwa uvumilivu na upendo na kwa uhakika mtulivu kwamba yote yangekuwa sawa.

Hii ni baraka ya nguvu ya Mungu, inayopatikana kwetu kupitia maagano matakatifu na kwa sababu ya dhabihu ya upatanisho ya Mwokozi. Nguvu hii inatubadilisha, inatuimarisha, inatutuliza, inatupa kujiamini, hutuletea amani, na huongeza uwezo wetu wa kutimiza majukumu yetu matakatifu kama wanawake.