“Urejesho wa Sakramenti,” Liahona, Machi 2025.
Njoo, Unifuate
Urejesho wa Sakramenti
Wakati Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ilipoanzishwa mnamo 1830, Bwana alirejesha ibada takatifu ya sakramenti. Aliwaamuru watu Wake “kukutana pamoja mara kwa mara ili kupokea mkate na divai katika ukumbusho wa Bwana Yesu” (Mafundisho na Maagano 20:75).
Ratiba hii inaonyesha jinsi sakramenti ilivyoanzishwa katika zama tofauti. Ingawa watu na mahali hubadilika, katika kila zama sakramenti huwasaidia wanafunzi wa Yesu Kristo daima kumkumbuka na kuwa na Roho Wake pamoja nao.
|
Agano Jipya |
Kitabu cha Mormoni |
Mafundisho na Maagano |
Siku yetu |
Wakati Yesu Kristo atakapokuja tena | |
|
Ambao |
Yesu Kristo na Wanefi |
Joseph Smith na waumini wa kwanza wa Kanisa la urejesho la Yesu Kristo |
Watakatifu wa Siku za Mwisho ulimwenguni kote |
Yesu Kristo na “wale wote ambao Baba [Yake] amempa [Yeye] kutoka ulimwenguni” (Mafundisho na Maagano 27:14) | |
|
Nini |
Mkate na divai kwa ukumbusho wa mwili na damu ya Yesu (ona Mathayo 26:26–28; Marko 14:22–24; Luka 22:17–20) |
Mkate na divai kwa ukumbusho wa mwili na damu ya Yesu (ona 3 Nefi 18) |
Mkate na divai, vikibarikiwa kwa sala mahususi zinazopatikana katika Mafundisho na Maagano 20:77, 79 |
Kwa kawaida mkate na maji, vikibarikiwa kwa sala maalum zinazopatikana katika Mafundisho na Maagano 20:77, 79 |
Mkusanyiko ulioongozwa na Yesu Kristo, ambapo Yeye “atakunywa matunda ya mzabibu pamoja [nasi] duniani” (Mafundisho na Maagano 27:5) |
|
Lini |
Ilianza karibia miaka 33 B.K, usiku ule kabla ya Kusulubiwa kwa Yesu Kristo |
Ilianza karibia miaka 33 B.K baada ya Ufufuko wa Yesu Kristo |
Ilianza wakati Kanisa lilipoanzishwa Aprili 6, 1830 … |
Kila wiki katika mikutano ya sakramenti |
Wakati Yesu Kristo anapokuja tena duniani |
|
Wapi: |
Katika “chumba kikubwa orofani” cha nyumba iliyoko Yerusalemu (Marko 14:15) |
Katika “nchi ya Neema” (3 Nefi 11:1) |
Katika nyumba ya Whitmer huko Fayette, New York, Marekani |
Katika nyumba za mikutano ulimwenguni kote |
“Duniani” (Mafundisho na Maagano 27:5) |
|
Kwa nini |
Kuwapa watu nafasi ya kumkumbuka Yesu Kristo na “kufanya upya agano lao la kujichukulia juu yao jina la Mwokozi, ili daima kumkumbuka Yeye, na kushika amri Zake.” | ||||
Tafakari
Ni kwa jinsi gani kujua lengo la sakramenti kunaimarisha uhusiano wako na Yesu Kristo?