2025
Njia 7 za Kufurahia Muziki Wenye Mwongozo wa Kiungu
Machi 2025


“Njia 7 za Kufurahia Muziki Wenye Mwongozo wa Kiungu,” Liahona, Machi 2025.

Njoo, Unifuate

Mafundisho na Maagano 25

Njia 7 za Kufurahia Muziki Wenye Mwongozo wa Kiungu

“Fanya uchaguzi wa nyimbo takatifu … “Kwani nafsi yangu hufurahia katika nyimbo za moyoni” (Mafundisho na Maagano 25:11).

mwanamke akiangalia simu ikiwa na wimbo kwenye skrini

Picha na David Green

Wakati wote, muziki umekuwa sehemu muhimu ya kuabudu kwa wanafunzi wa Yesu Kristo.

Zaburi nyingi katika Agano la Kale ni nyimbo za sifa kwa Bwana. Agano Jipya linaandikwa kwamba Yesu na Mitume Wake, kabla ya kuelekea Gethsemane, waliimba wimbo pamoja (ona Mathayo 26:30). Na nyimbo huboresha kuabudu kwetu wakati wa mikutano ya sakramenti leo.

Uumbaji unaoendelea wa kitabu kipya cha nyimbo za dini ni wa kusisimua, na tunaweza kutazamia nyimbo zaidi zilizo mpya wakati mchakato unaposonga mbele. Lakini nyimbo za dini sio aina pekee ya muziki ambao unaweza kutuvutia. App za Maktaba ya Injili ya Kanisa na Muziki Mtakatifu zina aina nyingi tofauti za muziki wa kuufurahia, kutoka kwenye muziki wa jadi wa kwaya hadi muziki kucheza, na wa kisasa (huhitaji kuwa kijana ili kufurahia albamu ya Strive to Be!). Ndani ya app hizi unaweza kupata rekodi chanya, rekodi za kuvutia, nyingi ambazo zinajumuisha muziki wa karatasi unaoweza kucheza au kuimba mwenyewe.

Haya ni baadhi ya mawazo ya kukusaidia kujumuisha muziki wenye mwongozo wa kiungu katika kuabudu kwako nyumbani—hata kama huna mafunzo ya muziki:

  • Sikiliza rekodi za nyimbo za dini na nyimbo zingine zenye mwongzo wa kiungu kwa wiki nzima. Hizi zinaweza kupatikana katika app za Maktaba ya Injili au App ya Muziki Mtakatifu au katika Maktaba ya Muziki kwenye tovuti ya Kanisa.

  • Chunguza hadithi za nyimbo na ujifunze kile kilichowavutia.

  • Imba nyimbo za dini na jifunze sehemu tofauti ukitumia chaguo la Maingiliano ya Muziki kwenye App ya Muziki Mtakatifu au kwenye tovuti ya Kanisa.

  • Sikiliza Kwaya ya Tabernacle au Jitahidi Kuwa kwenye jukwaa lako unalolisikiliza (kama vile YouTube, Spotify, Apple Music, Pandora).

  • Jifunze kucheza nyimbo za dini na nyimbo zingine zenye mwongozo wa kiungu kwenye kinanda au gitaa kwa kutumia karatasi ya muziki au nyimbo zilizojumuishwa kwenye app ya Maktaba ya Injili au kwenye tovuti ya Kanisa.

  • Jifunze na utafakari mashairi ya nyimbo za kuinua na nyimbo za dini.

  • Fuatilia pamoja na mashairi wakati mkisikiliza maonyesho ya Kwaya ya Tabernacle kwenye Temple Square. Maonyesho yanaweza kupatikana kwenye chaneli ya YouTube ya kwaya.