“Huduma ya Mitume: Kazi Ambayo Hakuna Mwingine Anayeweza Kufanya,” Liahona, Machi 2025.
Huduma ya Mitume: Kazi Ambayo Hakuna Mwingine Anayeweza Kufanya
Jinsi gani huduma ya ulimwenguni kote ya Mitume wa sasa wa Bwana inavyowagusa watu kwa wema.
Akidi ya Mitume Kumi na Wawili inasimama kama mashahidi wa Yesu Kristo ulimwenguni kote. Wito wao ni wa kipekee na wenye uzito. Baada ya kuitwa kuhudumu, wanafunga milango kwenye kazi zao maarufu ili kuweka wakfu muda wao wote na vipaji vyao ili kuwabariki wengine. Kila moja huleta vipawa na vipaji vya kipekee kwenye wito wao, vilivvyochngwa na huduma ya maisha yote, kufundisha na kujifunza injili, na kushinda changamoto kwa imani katika Bwana.
Mzee Ronald A. Rasband wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili na mke wake, Melanie, walikuwa wamekaa tu kwenye viti vyao kusikiliza burudani ya muziki wa Krismasi wa shule ya mjukuu wao wakati mkuu wa shule alipowakaribia na kuomba kama Mzee Rasband angewakaribisha hadhira.
Alipokuwa akisimama na kutazama umati ule na bendi—wote wakiwa na shauku ya kuanza—yeye alifikiria kuwakaribisha tu wageni na kuwatakia jioni ya njema. Lakini kisha akakumbuka wito wake wa kitume daima kusimama kama shahidi maalum katika mahali pote. “Mabibi na mabwana,” alisema, “Siwezi kukosa fursa [ya haya] majira ya kuzaliwa kwa Kristo ili kutoa ushuhuda wa jina Lake na huduma Yake.”
Po pote waendapo, ye yote wanayekutana naye, ujumbe wa Mitume ni uthibitisho wa Yesu Kristo kama Mwana mkombozi wa Mungu. “Kwanza kabisa, wakati wote, sisi ni mashahidi wa uhalisia wa uhai wa Bwana Yesu Kristo,” alisema Mzee David A. Bednar.
“Yesu Kristo ndio sababu ya sisi kuwa hapa,” Mzee Dale G. Renlund aliwaambia akina dada wa Muungano wa Usaidizi katika ibada jijini London mwaka jana. Ninajua kuwa Yeye yu hai. Muujiza halisi hutokea katika maisha yako unapojua hilo wewe mwenyewe.”
“Ninawezaje kusaidia kujenga imani yao katika Yesu Kristo?” alisema Mzee Quentin L. Cook kwa waumini huko Sydney, Australia, akisimulia jinsi swali hilo lilivyotengeneza jumbe zake kwa miaka mingi.
Mafundisho yao yanaonyesha hisia ya uharaka na kutamani wanakohisi kwa wengine kuinuka katika utakatifu ili kumwona na kumhisi Mwokozi na kupata uzoefu wa neema Yake ya kulipia dhambi (ona 3 Nefi 11:15). Mafundisho yao yamelowanishwa katika upendo na uelewa. Ombi lao la kutubu bado ni la upole lakini imara. Hamu yao kwa waumini ya kukua katika mambo ya Mungu ni dhahiri kama isivyoweza kukanushika. Wakati watu wanaposikia ushuhuda uliotolewa na Mtume, mioyo inaweza kuguswa na maisha kubadilishwa.
Mashahidi wa Yesu Kristo
Kila Mtume huleta talanta za kipekee na uzoefu wa kushuhudia katika kazi yake. Kila mmoja alikuwa mashuhuri katika taaluma ya kazi yake. Kila mmoja ni tofauti katika utu na mtindo, lakini wanashiriki sifa za kawaida. Wana furaha, ni chanya, na wanaondoa shaka ya kuwepo. Mara nyingi, wale wanaokutana na Mtume wa Yesu Kristo wanavutiwa na heshima yao na asili halisi.
Kuna uharaka kuhusu Mitume kufanya mambo yafanyike—ari ya kubariki, kuleta faraja, na kutoa ushuhuda.
“Kwa miongo mitatu, imekuwa heshima yangu na fursa ya kujumuika na washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho,” alisema Rais Jeffrey R. Holland, Kaimu Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. “Bila ubaguzi, kila mmoja wa watu hawa amenisaidia kuwa mfuasi bora wa Yesu Kristo.
“Tulipokusanyika hivi karibuni kupiga picha ya akidi, nilihisi hisia za shukrani kubwa kuwa sehemu ya utaratibu unaoendelea wa wafuasi wa kale na wa kisasa wa Yesu Kristo.
“Majina na nyuso … katika akidi hili hubadilika baada ya muda, lakini kile ambacho ni muhimu hubakia: kila mtume amekubali jukumu la ‘kuwa shahidi maalum wa jina la Kristo ulimwenguni kote’ [ona Mafundisho na Maagano 107:23]. Hakuna kazi tamu iliyoweza kutolewa kwa yeyote, wala kundi lolote zuri la wanadamu ambalo kwalo litaifanya.”
Mzee Dieter F. Uchtdorf anazungumza wakati wa mkutano maalumu wa Wilaya ya Yerusalemu katika Kituo cha Yerusalemu cha BYU mnamo Aprili 22, 2023.
“Hisia za shukrani kwa Mwokozi zilinizidia leo wakati tukifikiria dhabihu Yake katika maeneo mawili maalumu,” alisema Mzee Dieter F. Uchtdorf, wakati akizuru maeneo matakatifu katika Israeli mwaka 2023. “Tulitembelea Kaburi la Bustani,” mahali ambapo yawezekana mwili wa Kristo ulilazwa.
“Tulitembelea pia eneo lililofikiriwa na baadhi kuwa Bustani ya Gethsemane. Tulipokuwa tukitembea miongoni mwa miti ya mizeituni ya karne nyingi, tulisikiliza mistari ya maandiko ikielezea dhabihu takatifu ya Mwokozi kwa niaba yetu katika bustani hii na msalabani
“Uzoefu wa maumivu makali wa Yesu Kristo katika Bustani ya Gethsemane na juu ya msalaba unastahili heshima yetu kamili na staha kamili. Vivyo hivyo, matukio ya ajabu yaliyotokea siku ya tatu kufuatia kusulubiwa Kwake yanastahili kuchukua nafasi ya hofu na shukrani za milele ndani ya mioyo na akili zetu.
“Kama mfuasi wa Kristo, nimebarikiwa kutangaza ushuhuda wangu kwamba Yeye yu hai!”
Katika makala ya mitandao ya kijamii kuhusu unyenyekevu kwa Bwana, Mzee Gerrit W. Gong alihimiza, “Na daima tuzungumze kwa upendo na shukrani za staha kwa kazi na utukufu wa Mungu na matendo mema, rehema, na neema ya Yesu Kristo na dhabihu Yake ya kulipia dhambi.”
Kumtayarisha Mtume
“Inamchukua Bwana muda mrefu kumtayarisha Mtume,” Rais Russell M. Nelson alisema. “Wakati mtu huyo anapoitwa katika Wale Kumi na Wawili, Bwana ana kitu cha kipekee ambacho Yeye anatarajia mtu yule kuchangia.”
Katika njia ya kila Mtume huja majaribio—“mitihani katika ujasiri na subira”—daima roho ikitafuta, wakati mwingine ya kutishia maisha.
“Daima kuna jaribio,” Rais Nelson alisema, akielezea kazi katika huduma ya Bwana. “Je, uko tayari kufanya mambo magumu kweli kweli? Mara unapokuwa umeonyesha utayari wa kufanya sehemu yako, Yeye atakusaidia.”
Wakati akihutubia waumini huko Australia, Mzee Cook alitoa taswira ya uzoefu wake kwa kusimulia jinsi washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili wamejisikia kutokujiandaa na hawatoshi kama vile viongozi wa kata wakati mwingine wanavyojisikia. “Kuwa Mtume, katika huduma ya Bwana, ni ya kunyenyekeza sana,” alisema.
Kama Mtume mpya aliyeitwa, Mzee Neil L. Andersen alieleza kwamba ingawa alijisikia mpungufu na mnyenyekevu, alipata faraja kwamba Bwana alikuwa amembariki na angalau sifa moja: “Ninajua kwa ukamilifu na uwazi dhahiri kupitia nguvu ya Roho Mtakatifu kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana Mpendwa wa Mungu.”
“Nimeulizwa unajisikiaje kuwa Mtume mpya zaidi,” alisema Mzee Patrick Kearon siku ile baada ya wito wake kwenye Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.
“Nimekuwa na hisia zote za kufikirika, na ninajua hii ni zaidi yangu mimi. Lakini nitaomba msaada. Ninaamini kabisa katika Baba wa Mbinguni mwenye upendo na Mwanawe, Mwokozi wetu. Na ninajua kwamba Wao watanisaidia; Na mimi ninategemea hilo. Na nitafanya kadiri niwezavyo kuwa, baada ya muda, kitu fulani katika mistari ya Mtume ambacho mnaweza kuwa nacho katika mawazo yenu.
“Na hivyo siku hii wakati ninahangaika, masaa 24 baada ya wito, kuja katika maelewano na hili, ikiwa una siku ambayo unahisi umenyooshwa … zaidi ya mawazo yako yasiyofikirika, vyema, niko pale pamoja nawe.”
Rais Russell M. Nelson aliongoza ujumbe wa viongozi wa Kanisa, ikijumuisha Mzee Gerrit W. Gong, katika kuwatembelea mfalme na malkia wa Tonga mwaka 2019. Mitume wanakutana na waheshimiwa na wakuu wa nchi katika jukumu lao la kufungua milango ya mataifa kwa injili. Miaka mingi inahitajika ili kuwaandaa Mitume kwa kazi yao kuu, alisema Rais Nelson.
Mabalozi kwa Ulimwengu
Akirejelea Mafundisho na Maagano 107:23, ambapo Bwana anawaita Mitume Kumi na Wawili kuwa “mashahidi maalumu wa jina la Kristo ulimwenguni kote,” Rais Nelson alisema: “Kila mshiriki wa Wale Kumi na Wawili ni Mtume kwa ulimwengu wote. Anahitaji kujifunza kuhusu kila sehemu ya ulimwengu, pamoja na watu na lugha na historia.”
Kazi yao inasambaa ulimwenguni. Wanakutana na wakuu wa nchi, waheshimiwa wenyeji, vyombo vya habari, na waumini wa Kanisa katika mazingira makubwa na ya kibinafsi. Masaa yanaweza kuwa marefu na mahitaji makubwa. Kama mabalozi wa Bwana Yesu Kristo, maisha yao sio yao tena.
Wakati wa ziara iliyokuwa na ratiba nyingi ya huduma ya ulimwengu kwa mwaka uliopita, ya siku 12 kupitia nchi sita za Ulaya—ambapo kulala mara nyingi kulikuja wakati wa safari ya usiku kati ya nchi—Mzee D. Todd Christofferson alikutana na viongozi wa serikali, wamisionari, na waumini wa Kanisa wa eneo hilo.
Ya kukumbukwa ilikuwa mkutano na Waziri wa Utamaduni na Vyombo vya Habari huko Croatia, ambapo alitoa msaada wa Kanisa ili kuwasaidia wakimbizi wengi wanaofurika katika nchi yake kutokana na vita vya Ukraine. “Sisi … tuligundua kwamba kulikuwa na njia nyingi tofauti … tungeweza kushirikiana, hasa [katika kuwasaidia] wale walio katika shida kubwa,” Mzee Christofferson alisema.
Baada ya kuzungumza na viongozi wa maeneo husika jijini Dar es Salaam, Tanzania, akitangaza mchango wa Kanisa kwenye mradi mkubwa wa kibinadamu mwaka 2024, Mzee Gary E. Stevenson alikutana na waumini na wamisionari.
Wakati wa safari ya siku tisa kwenda nchi kadhaa za Afrika mwaka jana, Mzee Gary E. Stevenson alitembelea Kituo cha Afya cha Makuburi jijini Dar es Salaam, Tanzania, mahali ambapo Kanisa linasaidia kupanua kituo hicho. “Tunapoona huduma ambayo inatolewa kwa akina mama na watoto hapa,” alisema Mzee Stevenson, “mioyo yetu inaguswa.”
Ili kuadhimisha miaka 30 ya Kanisa huko Cambodia, Mzee Renlund alikutana na waziri mkuu wa Cambodia, ambaye alimwelezea kama “mtu wa ajabu.”
Mtume, aliyekuwa mtaalamu wa moyo, alimwambia waziri mkuu kwamba Kanisa la Yesu Kristo lilikuwa likichangia karibu dola za Marekani milioni 2.2 ili kwamba kituo cha moyo kiweze kuongezwa katika hospitali huko Siem Reap, iliyoko takribani maili 200 (320 km) kaskazini mwa Phnom Penh, ili kuleta huduma bora ya afya kwa wale kama mjomba wa waziri mkuu, ambaye alikufa kutokana na ugonjwa mkali wa moyo.
Mzee Dale G. Renlund akisalimiana na Samdech Moha Borvor Thipadei HUN Manet, Waziri Mkuu wa Ufalme wa Kambodia, huko Phnom Penh mnamo Januari 22, 2024. Mkutano wa kihistoria ukiwakilisha mara ya kwanza kwa kiongozi wa Kanisa kukutana na kiongozi mkuu wa serikali ya Ufalme wa Kambodia.
“Nilikuwa na fursa ya kuwa na waumini, viongozi, na wamisionari huko Ulaanbaatar, Mongolia, na huko Kyoto, Hiroshima, Fukuoka, Sapporo, na Tokyo, Japani,” alisema Mzee Ulisses Soares baada ya kutembelea Eneo la Asia Kaskazini mwaka 2024. “Katika kila mkutano au muingiliano binafsi, nilihisi upendo wa ajabu na imani ambayo watu hawa wanayo kwa Bwana. Hadithi zao za ajabu za uongofu zilinigusa kwa kina na kuimarisha ushuhuda wangu juu ya Yesu Kristo na injili Yake ya urejesho duniani.
“… Ilikuwa baraka iliyoje kwangu kuhisi Roho wa Bwana na upendo Wake miongoni mwa wafuasi hawa wakuu wa Kristo katika nchi hizi.”
Kazi ya Mitume
Kufungua milango kwa ajili ya injili katika nchi mbalimbali ni jukumu muhimu la kitume: “Hawa Kumi na Wawili wakiwa wametumwa, wakishikilia funguo, za kufungua mlango kwa tangazo la injili ya Yesu Kristo” (Mafundisho na Maagano 107:35).
Katika uzoefu wa Rais Nelson kama mshiriki wa Wale Kumi na Wawili, milango ya injili imefunguliwa tofauti. Wakati mwingine Roho alimfanyia kazi kiongozi wa serikali hadi “akaanza kubadili mawazo yake kutuhusu sisi,” Rais Nelson alisema. Wakati mwingine mtu ambaye hakuwa tayari kuzungumza na viongozi wa Kanisa aliondolewa ofisini, na Bwana alitupatia “mtu ambaye tungeweza kuongea naye.” Katika kila hali, Rais Nelson alisema, “ujumbe [kutoka mbinguni] kwangu ulikuwa sawa: ‘Fanyeni kwa moyo wako. … Thubutu. Kisha wakati hauwezi kwenda mbali zaidi, nitakusaidia.’”
Shangwe ya kazi ya Mtume, wanasema, inakuja wakati wa kusawazisha mahitaji yenye changamoto ya kuzungumza na makundi makubwa na pia kuhudumia mtu binafsi. Wanawatembelea waumini katika nyumba zao ili kutoa baraka, kuonyesha shukrani, au kutoa ushauri unaohitajika.
Mzee Bednar alisema: “Bwana humtuma mshiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili katika sehemu maalumu kwa wakati maalumu ambapo tunakutana na Watakatifu wa Siku za Mwisho waaminifu na wengine ambao mara nyingi wanasumbuka au wanahitaji faraja na hakikisho. Mungu huyapanga maingiliano hayo.
Mzee David A. Bednar na mkewe, Susan, wanasalimiana na watu baada ya kuzungumza katika mkutano huko Toluca, Mexico, mnamo Novemba 5, 2023.
Wakati mwingine huduma yao ni kwa umma hasa, kama vile wakati Mzee Stevenson aliposhiriki katika mkutano mkuu wa habari jijini Nairobi, Kenya, ambao ulitangazwa kwenye televisheni ya taifa ya moja kwa moja. “Swali ambalo linaweza kuwa kwenye … Akili zenu ni zipi, ‘Mtume ni nini?’” Mzee Stevenson alisema wakati wa matangazo hayo. “Sisi … tumeitwa kwenda katika mataifa ya ulimwengu na kutoa ushuhuda wa Uana mtakatifu wa Yesu Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.”
“Yote ni kuhusu Yeye,” alisema Mzee Dieter F. Uchtdorf. “Tunamwakilisha Yeye. Yote ni kuhusu Mungu na ukuu Wake na umuhimu Wake kwa ajili ya furaha ya watoto Wake.”
Kazi yao wakati mwingine iko karibu na nyumbani—kiuhalisia. Mzee Bednar alikuwa akifanyia matengenezo paa la nyumba yake siku moja na akaenda kwenye duka la mtaani hapo kununua vifaa kadhaa. Alikuwa amevaa nguo za kazi: suruali ya kawaida na viatu, shati, na kofia ya baseball.
“Mtu alinikaribia nilipokuwa nikichagua vifaa vyangu na kusema, ‘Mzee Bednar, kujificha hakufanyi kazi.’ Tulicheka, na kisha akauliza, ‘Je, wewe utajalii kama nitakuuliza swali?’
“Nilijibu, ‘Naam, hiyo ndiyo sababu niko hapa.’
“Alijibu kwa maswali, ‘Unamaanisha nini?’
“Nilisema, ‘… Nipo hapa kwa sababu Mungu alijua tungekutana katika duka hili na kwamba ulikuwa na kitu fulani ambacho ulitaka kuuliza Tafadhali nenda mbele na ushiriki nami swali lako.’
“Tulizungumza katika njia kwa takribani dakika 15, na nilijaribu kumsaidia kupata jibu la swali lake. Je, ilikuwa ni bahati tu kwamba nilikutana na mtu huyu mwema kwenye duka la mtaani kwetu? Au ilikuwa tukio hili takatifu lililoanzishwa na Mwokozi mwenye upendo ambaye … alijibu wasiwasi wa mtu mwaminifu—mmoja?
“Ninaamini kwamba katika kazi ya Bwana hakuna kitu kama bahati nasibu. Thamani ya nafsi ni kubwa machoni pa Mungu.”
Mzee Neil L. Andersen anasimama kupigwa picha mnamo Februari 22, 2024, katika Kijiji cha Jaime Cardinal Sin, Manila, Ufilipino, ambako Kanisa lilikarabati matangi matatu ya maji.
Kukabiliana na Changamoto kwa Imani katika Bwana
Matatizo makubwa na magumu yanawakabili Mitume wa leo. Wanatafuta mwongozo wa kiungu wanapofundisha na kutumikia mkusanyiko wa ulimwenguni kote wa waumini wa Kanisa zaidi ya milioni 17 wanaojaribiwa na changamoto kama machafuko ya kisiasa, ponografia, mashinikizo ya mitandao ya kijamii, au kutokuwa na uhakika wa kiuchumi. Migogoro kati ya mataifa inavuruga kazi. Changamoto za momonyoko wa maadili ya jadi unatoa kwa utulivu wa kijamii.
Washiriki wa Wale Kumi na Wawili wanatulizwa na majukumu yao na wana hamu ya kujenga imani katika ulimwengu usio na imani.
“Ni wazi nguvu za Bwana zinatembea juu ya viongozi wa Kanisa, zikiwagusa kwa kiwiko na … uharaka,” alisema Rais M. Russell Ballard (1928–2023), Kaimu Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. “Swali ambalo lazima sote tujiulize ni, ‘Je, tunaendelea mwendo sawa na [viongozi wetu]?’ Kila mmoja wetu lazima awe tayari kujibu swali hilo. Ninaweza kuwahakikishieni kwamba ni mada ya mjadala mkubwa miongoni mwa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. … Huu sio wakati wa kupumzika au kufika pwani katika miito yetu. …”
“… Lazima tuwe tayari kuweka kasi sawa na viongozi wetu, kurefusha hatua kwa kila hatua yao ndefu.”
“Kama wafuasi wa Yesu Kristo, tunatafuta kuwa kama Mwokozi wetu na kufuata mfano Wake katika yote tunayofanya,” alisema Mzee Uchtdorf. “Kutoka wakati ule tunapoweka mguu juu ya njia ya ufuasi, baraka zinazoonekana na zisizoonekana kutoka kwa Mungu zinaanza kutufikia.
“Bila kujali mahali tulipo, wewe na mimi tunaweza kutembea katika njia ya ufuasi leo. Na tuwe wanyenyekevu; acha tuombe kwa Baba yetu wa Mbinguni kwa mioyo yetu yote na kuonyesha hamu yetu ya kusogea karibu Naye na kujifunza juu Yake.”